Thursday, August 14, 2014

Wema Sepetu Ni Mpenda Starehe Na Mashoga Wapenda Anasa: Diamond Platnumz

Diamond na Wema Sepetu
Baada ya Team Wema kumshukia Diamond kwenye mitandao ya kijamii kuwa Diamond ndiye anayemshusha Wema Sepetu badala ya kumuendeleza. Diamond amefungukia habri hiyo kwa kusema Wema ndiye mwenye matatizo mwenyewe kwa kutotaka kufanya akzi na kupata maendeleo badala yake kuendekeza starehe na mashoga wapenda starehe. Kupitia Instagram Diamond ameandika

"Nafkiri ningewaona kweli Mna akili na Mapenzi ya dhati kwa Msanii wenu... kama mngemshauri apunguze Mashoga wapenda anasa na apunguze Starehe zisizo na Faida, huenda ingemsaidia Pesa kuzitumia kwenye kufanya kazi na kuleta maendeleo badala ya kuwapa viwanda vya pombe... Mimi kama bwana, wajibu wangu ni kuhakikisha Mpenzi wangu anakula vizuri, anavaa vizuri, analala vizuri, na kumuwezesha mtaji wa kufanyia kazi.... Waswahili wanasema Mchungaji bora anatakiwa kuhakikisha anampeleka Ng'ombe wake Kwenye Maji safi....ila yeye ng'ombe mwenyewe ndio anatakiwa aamue kunywa maji!!!!! Au mnataka nikishampa mtaji niache kufanya na show tena na kuigiza nimuigizie mie ???? Nisiende Studio nikae dukani nimuuzie mie????.. ni juhudi zako kwanza!... leo hii mimi Hata ningepewa Mamilioni ya mamilioni kama nisingekuwa na moyo wa mie mwenyewe kwanza kutaka kujituma na kupenda kufanya kazi yangu nisingefikia hapa nilipo!....Mxieeeeeeeew!emoji Kama nimekuchefua Lamba ndimu Usitapike emoji"

Hivi karibuni baada ya tuzo za MTV Africa Music Award 2014 ambazo Diamond na Wema walihudhuria baada ya kurudi Diamond wakati akifanyiwa interview na radio moja nchini alisema kuwa amemuunganisha Wema na wadau muhimu wa filamu toka Ghana ili aanze kufanya filamu kimataifa ba sio Tanzania pekee lakini Wema mpaka sasa yupo kimya .




No comments:

Post a Comment