Wednesday, July 23, 2014

Wema Sepetu Aharibika Ngozi, Ashindwa Kutoka Nje Na Kukataa Kupigwa Picha !

Wema Sepetu amesikitishwa na kitendo cha ugonjwa wa ngozi uliomtokea sasa sehemu ya shavu lake la usoni kiasi cha kuharibu urembo wake na kushindwa kutoka nje. Akizungumza na GPL Wema alisema kuwa kipele hicho kilianza kama mzaha na baadaye akaenda hospitali kupewa dawa lakini kikazidi badala ya kutoweka
"Ulianza muwasho, kikawa kipele kisha kikageuka kama kishilingi.
Nilipokwenda hospitali nilipewa dawa ya crime ya kupaka, mimi nikachua eneo lililoathirika, kumbe ndiyo nikawa nasababisha matatizo, kukavimba zaidi kama unavyoona,” Alisema Wema huku akikataa kupigwa picha na paparazi

No comments:

Post a Comment