Tuesday, June 24, 2014

Wema Sepetu Hembu Tuachie Na Sisi Huyo Diamond: Baby Madaha

Baby Madaha
Star wa filamu na muziki wa Bongoflava Baby Madaha anadaiwa kuwewesekea penzi la Diamond Platnumz na kumtaka Wema Sepetu awaachie na wao Diamond a.k.a Sukari ya warembo ili wafaidi kama anavyojiachia Wema. Chanzo kimoja kilicho karibu na Baby Madaha ambacho pia kinafanya juu chini kuwika katika filamu kwa masharti ya kutotajwa jina lake kikizungumza na Swahiliworldplanet wiki iliyopita kilisema kuwa

"Nawapa habari, Baby Madaha anamtaka Diamond hata kule kumponda kwenye media sio kwa dhati ni njia ya kumshawishi amtokee na kufanya kweli, sikia nikuambie katika Kill Awards(mwaka huu) Madaha alikuwa na lengo la kumbusu Diamond kwa stage but alikuwa anamhofia Wema na Team Wema wangeweza kuja juu ikawa habari mpya, anamtaka ila anashindwa tu kusema wazi unajua Wema anambana sana Diamond, anataka Wema amwachie" kilisema chanzo hicho huku kikisisitiza kuwa kisitajwe jina lake hata kwa dawa.

Baada ya kupata habari hiyo wiki iliyopita SWP ilijaribu kumsaka Baby Madaha na alipopatika na kuulizwa alionekana kushangaa kwa kusema "Siko Tz na wala sikuwepo tuzo za Kill, wrong info"

Baby Madaha na Diamond
Like our Facebook page Swahili World Planet for more updates about Tanzanian movie stars' latest gossips, news, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news

No comments:

Post a Comment