Wakati mastaa wengi wa kike na wa kiume katika tasnia ya filamu nchini wakiwa wamejiachia sana kunenepeana kiasi cha kuwawia vigumu kupendeza wanapovaa nguo kwenda kwenye events mbalimbali ikiwemo kwenye red carpet lakini ni tofauti kwa Irene Paul ambaye amekuwa makini sana kutoruhusu mwili wake kunenepeana bila sababu za msingi. Irene Paul amekuwa na figure yake ya ki-miss ambayo mastaa wenzake wengi wamekuwa wakiimezea mate kwani mara nyingi anapovaa nguo kwenye events hasa red carpet hupendeza hata anapopigwa picha hutoka vizuri tofauti na baadhi ya mastaa wenzake wengi ambao hata kama wamevaa nguo nzuri huangushwa na miili yao iliyonenepeana hovyo.
Hata hivyo
Swahiliworldplanet imefanikiwa kugundua siri ya kinachomfanya star huyo kuwa na figure hiyo, habari za uhakika zisizo na shaka ni kuwa Irene Paul anatumia diet maalum ya products za Aloe Vera ambazo inadaiwa hazina madhara ingawa ni vizuri mhusika kumuona daktari kwanza kabla ya kuanza kutumia. "Irene ana umbo zuri kwasababu anatumia diet maalum ya bidhaa za Aloe vera, unajua Irene hapendi kunenepa hovyo ndiyo maana yupo kwenye shape kwa muda mrefu" kilisema chanzo kimoja cha kuaminika ambacho kipo karibu na star huyo wa filamu za Love Power, Handsome Wa Kijiji na Unpredictable.
Muigizaji kuwa na umbo la kawaida na kufanya mazoezi na diet mara kwa mara si tu kuwa humfanya apendeze kirahisi anapovaa nguo mbalimbali bali humfanya pia kuwa rahisi kucheza characters mbalimbali kwa urahisi katika filamu bila kusahau kuwa mazoezi na diet nzuri humlinda mtu na magonjwa hivyo kuwa fit kiafya muda wote.
|
Irene Paul |
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Filamu kali ya SIO SAWA inaingia sokoni Ijumaa hii April 2014 hakikisha unanunua nakala yako halisi.
Follow us on twitter Swahili World Planet and Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies SWP for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities, features, beauty, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news, life styles news and
No comments:
Post a Comment