Friday, March 21, 2014

Lulu Kuolewa Na Mwarabu Tajiri Wa Mafuta Toka Dubai, Amwahidi Kumnunulia Gari Na Jumba La Kifahari.

Lulu
Habari mpya ni kuwa Star wa filamu Swahiliwood  mwenye jina kubwa kuliko umri wake Elizabeth Michael "Lulu" amemdatisha tajiri wa mafuta mwenye asili ya kiarabu ambaye ana makazi yake Dubai. Kwa mujibu wa Visa mwarabu huyo ameoza kwenye penzi la Lulu hivyo anataka kumuoa kabisa huku akimuahidi kumnunulia gari na jumba la kifahari. Habari zaidi zinasema kuwa muaribu huyo kwasasa ameweka kambi jijini Dar es salaam huku akimtumia Dr.Cheni ili amshawishi Lulu akubali ombi lake la kumuoa, imefikia hata Dr.Cheni ametishwa na kasi ya tajiri huyo wa mafuta kutaka kumuoa Lulu. Hata hivyo inadaiwa kikwazo ni dini kwani Lulu hataki kubadili dini na kuwa muislamu huku tajiri huyo akitaka kufunga ndoa ya kiislam na Lulu.
Kikizungumza na gazeti hilo chanzo kilisema "Anamtumia Dr.Cheni ili aweze kumshawishi Lulu lakini kinachofanya zoezi hilo kuwa gumu ni imani ya kikristu ya Lulu kwasababu Lulu hataki kubadili kabisa dini yake wakati jamaa anataka kumuoa kiislamu"

                                                                         Lulu

Follow us on twitter Swahili World Planet  and Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies SWP for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities, features, beauty, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news, life styles news and more

No comments:

Post a Comment