Friday, November 8, 2013

YUSUPH MLELA ADAIWA KUANZA KUPOTEA KWENYE FILAMU.

Yusuph Mlela ambaye ni star wa filamu Swahiliwood anadaiwa kuanza kushuka chati katika filamu tofauti na miaka miwili iliyopita.  Swahiliworldplanet wikiend iliyopita iliwashuhudia mastaa wanne wa filamu wakimjadili Mlela wakati wapo location wakirekodi filamu mpya wakisema Mlela kwasasa ameshuka chati sababu alijipandisha juu kwa kutaka pesa kubwa kwenye filamu na matokeo yake ameanza kupotea mapema sana. "kuna kipindi Mlela alijiona ni baabkubwa na kutaka dau kubwa kwenye filamu sababu ya kupata ustaa haraka, wakati bado alikuwa mchanga kwenye fani, matokeo yake waandaaji wengi wameanza kumpotezea na kwenye filamu sasa hivi haigizi sana kama mwanzoni" alisema msanii mmoja wa kiume

Nae muigizaji mwingine wa kike ambaye alishacheza filamu kadhaa na star huyo alisema hashangai sana maana industry ya filamu ni kama kupokezana kijiti kwa hiyo ukiwa juu leo kesho unaweza kushuka. "si unajua lakini hii industry ni kama kupokezana kijiti so ni kawaida tu"

Hata hivyo SWP ilimtafuta Mlela bila mafanikio ili atolee ufafanuzi madai hayo ya kudaiwa kuanza kupotea kwenye fani.

                                                                Yusuph Mlela
Follow us on twitter Swahili World Planet  and Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies SWP for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities, features, beauty, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news.

No comments:

Post a Comment