Friday, November 8, 2013

NIPO TAYARI KUCHANGIA PENZI LA DIAMOND PLATINUMZ NA WEMA SEPETU: VJ PENNY

Mtangazaji wa kituo cha televisheni cha DTV, Peniela Mwingilwa ‘Penny’, ambaye ni mpenzi wa mkali wa Bongo Fleva Diamond Platinumz amesema yupo tayari kuchangia mapenzi na msichana mwingine yeyote ambaye atachukuliwa na mwanaume huyo anayempenda.
Penny katika Penny na Wema.

Penny ambaye ni chaguo la mama mzazi wa staa huyo wa kibao cha My Number One, aliiambia Globalpublishers  maneno hayo, yanayotafsiriwa kama yupo tayari kuchangia mapenzi na hasimu wake, Wema Sepetu ambaye ni Miss Tanzania 2006n na muigizaji wa filamu Swahiliwood
“Ninampenda Diamond na sitaki kumpoteza. Nia yangu ni kumuona akiwa na furaha. Kama Diamond anaona kuna msichana mwingine wa kutoka naye na kwake hilo linampa furaha, basi mimi sina matatizo kwa sababu ninataka awe na furaha, nitaendelea kuwa naye,” alisema Penny.

Kumekuwa na habari zisizo na shaka kwamba Diamond na Wema wamerejesha uhusiano wao na hivi karibuni walitupia picha katika mitandao ya kijamii zilizowaonyesha wawili hao wakiwa katika mapozi ya kimahaba huko Ughaibuni.
Ingawa bado Diamond anatoka na Penny, lakini kwa siku za karibuni amekuwa karibu zaidi na mrembo huyo aliyetwaa taji la Miss Tanzania mwaka.

       Diamond Platinumz na Penny............................

Follow us on twitter Swahili World Planet  and Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies SWP for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities, features, beauty, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news.

No comments:

Post a Comment