LUPITA NYONG'O KAMA ANGEKUWA TANZANIA ASINGEWEZA KUPEWA NAFASI KATIKA FILAMU ZA KIBONGO.
 |
| Lupita |
Kipaji
cha kweli siku zote huonekana hata kama itachukua muda mrefu. Lupita
Nyong'o kutoka Kenya ameiteka Hollywood ndani ya muda mfupi tu kutokana
na performance yake hatari katika filamu ya 12 Years A Slave. Lupita
mwenye weusi hasa wa kiafrika au ule wa kisudani kila media nchini
marekani na nje zinataka kufanya nae interviews kuanzia majarida ya
filamu, mitindo na vipindi vya Tv vyote vinaonekana kutekwa na msanii
huyu chipukizi kutoka Africa mashariki. Filim critics wanampongeza kwa
performance yake kwenye hii filamu kiasi cha kutabiriwa nominations za
tuzo zote kubwa zikwemo Oscars katika kipengele cha Best supporting
actress, fashion critics nao hawapo nyuma kumpa kudos huku majarida yote
makubwa ya mitindo yakipigana vikumbo kufanya nae photoshoot na
interviews.
Hata kabla filamu ya 12 Years A Slave kutoka
nilivutiwa sana na trailer yake kwa kumuona Lupita labda kwa kuwa
napenda sana filamu za kihistoria zikiwemo za kuzungumzia Slave Trade na
baada ya filamu hiyo kutoka Lupita akawa an overnight star in
Hollywood. Am sure Lupita kama angekuwa hapa Tanzania(Bongo) asingepewa nafasi na
watengeneza filamu wa hapa kutokana na muonekao wake wenye asili ya
kiafrika hasa na umbo dogo la wastani, kwanza angeambiwa labda ajichubue
awe mweupe, anenepe awe na makalio ya kichina au umbo lake ni dogo
hawezi kucheza nafasi za mke wa mtu kama tulivyoshudia Mainda akiambiwa
umbo lake ni dogo ndiyo maana hapewi nafasi muhimu. Tunao kina Lupita
wengi tu hapa nchini lakini hawapewi nafasi eti hawauzi au wana sura
mbaya na hao wanaoitwa mastaa wa filamu vipaji hawana ila wapo kwa ajili
ya kukuza majina yao kwa skendoz na kuuza makava ya filamu.
Mfano
Jenifer yule mtoto aliyekuwa akiigiza na Kanumba na kuonyesha kipaji
cha hali ya juu na kuvuta mashabiki wengi mpaka nje ya nchi tayari
amepotea baada ya Kanumba kufariki lakini mtoto yule ana uwezo wa
kufanya maajabu hata Hollywood.
Lupita Leo hii tayari ni star mkubwa wa filamu kupitia filamu moja tu
tena akiwa amecheza kama mhusika msaidizi, amewamwaga mastaa wengi wa
Tanzania, Nigeria na Ghana kwa ustaa huko mtoni. Ukiachilia mbali kipaji
na muonekano wake wa asili kingine kilichomsaidia Lupita ni kuwa na
elimu nzuri katika tasnia ya filamu kwani amesomea mambo ya filamu. I
THINK muda umefika sasa kwa watengeneza filamu Tanzania kuangalia kipaji
cha kweli na sio uzuri wa sura na umbo kupewa kipaumbele kuliko kipaji
ili hata msanii akianza katika filamu zetu basi iwe rahisi kuwika
kimataifa akipata nafasi hiyo huku waigizaji wenyewe wakitakiwa kuongeza
elimu na bidii ya kazi. Hii ni kwasababu kuna wanaoitwa mastaa wakubwa
wa filamu Tanzania lakini hawana vigezo vya kuwika kimataifa wala vipaji
vyao havionekani licha ya kucheza filamu kibao, yaani umaarufu wao ni
mkubwa kuliko uwezo wao wa kuigiza.
Lupita akiwa katika filamu ya 12 Year A Slave........
Follow us on twitter Swahili World Planet and Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies SWP
for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities,
features, beauty, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and
Nollywood news.
No comments:
Post a Comment