Sunday, July 7, 2013

UHUSIKA KATIKA FILAMU YA TIKISA ULITAKA MTU KAMA KING MAJUTO: NISHA

Muigizaji maarufu wa filamu nchini Salma Jabu(Nisha) amesema kuwa filamu yake mpya ya "Tikisa" inayotarajiwa kuingia sokoni ijumaa hii inayokuja ni moto wa kuotea mbali hivyo mashabiki wa filamu za Kiswahili wasikose kujipatia nakala halisi ikiingia sokoni. Actress huyo machachari pia amesema kuwa kwa mara ya pili amecheza tena na King Majuto katika Tikisa baada ya kucheza wote katika Pusi na Paku kwakuwa script ya filamu hiyo ilitaka mtu wa aina ya King Majuto. Aliongeza kwa kusema kuwa haja-copy na ku-paste filamu hiyo na ndiyo maana amewashirikisha mastaa wengine kibao kama vile Jackline Wolper, Mboto, Hemed na Chuchu Hans. "nimeangalia script inataka nini,,na kwa character ya Tikisa majuto ndio ka-suit sana,,kuonyesha kuwa sijacopy na kupaste tikisa ndio maana TIKISA imechanganya wasanii mbali mbali km Hemed suleiman,Mboto,Chuchu Hans na Jackline Wolper na bila kunisahau mwenyewe Salma Jabu Nisha"

" Humo ndani kuna balaa na vionjo tofauti,,hakika kwa atakayeitazama ataona nini nazungumzia,,kamwe hutoijutia pesa yako kwa mnunuzi,,inatoka ijumaa ijayo,,si ya kuikosa hata wewe(Trim Saleem) uone ndani kuna nini na upate cha kui-challange NISHA'S FILM PRODUCTION" alimalizia Nisha


No comments:

Post a Comment