Sunday, July 7, 2013

IRENE UWOYA AKANA KUWA MAPENZINI NA FERE GOLA WA CONGO BAADA YA KUTUMIA JINA LAKE INSTAGRAM.

Irene Uwoya ambaye ni actress maarufu wa filamu za Kiswahili hivi karibuni alibadilisha jina lake instagram na kujiita IRENE WA FEREGOLA8 kitu ambacho kimesababisha baadhi ya watu wakiwemo mashabiki wake kuanza kuhisi kuwa muigizaji huyo na Fere Gola ambaye ni mwanamuziki maarufu wa Congo inawezekana ni wapenzi kwa siri ili watu hasa media zisijue na kuanza kuandika. Baadhi ya wasomaji wa Swahiliworldplanet baada ya kuona jina jipya analotumia Uwoya instagram waliujuza mtandao huu ili kumuuliza Uwoya kama yeye na Fere Gola ni marafiki wa kawaida tu au ni wapenzi?. SWP iliamua kumtafuta Uwoya na alipoulizwa kuhusu kutumia jina la mwanamuziki huyo instagram alijibu kwa ufupi "Namkubali sana ndo maana". Uwoya alipododoswa zaidi kama yeye na Fere Gola tayari walishakutana mara kadhaa labda na kupiga story za hapa na pale au amemfahamu kupitia kazi zake tu lakini bado hawajawahi kuonana actresss huyo ambaye ana mashabiki wengi nchini Congo hakujibu mpaka tunaandika habari hii. Angalia picha za wawili hao hapo chini...............

                          Fere Gola ambaye ni mwanamuziki maarufu Congo
Like our Facebook page Swahili World Planet for more updates about Swahili movies news, Gossip, features, reviews, celebrities and more, plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news

No comments:

Post a Comment