Monday, July 1, 2013

PLEASE! ! WAANDAJI WA FILAMU CHANGAMKIENI KUTUMA KAZI ZENU ZAFAA AWARDS 2013.


Hivi karibuni muandaaji wa kipindi maarufu cha The Sporah Show, Sporah Njau aishiye nchini Uingereza alichaguliwa kuwa mwakilishi wa Afrika Mashariki kwenye tuzo kubwa barani Afrika, ZAFAA Awards 2013.

bongo5 ilifanya  naye mahojiano ili kujua zaidi majukumu yake kwenye tuzo hizo. Mahojiano hayo yalikuwa kama ifuatavyo.

QN: Unadhani kwanini ulichaguliwa kuwa mwakilishi wa Afrika Mashariki?


SPORAH: Naamini sababu kubwa kabisa ni kwamba mimi mwenyewe ni mzaliwa kutoka Afrika Mashariki. Pili ni kwamba, nimekuwa kwenye TV screen za watu hapa Uingereza na Europe kwa ujumla kwa muda wa miaka zaidi ya 5, na kwajuhudi zangu zaidi nimebarikiwa kuwa mmoja wa wanawake wenye ushawishi mkubwa hapa Uingereza. I have amassed a great fortune through my media interests and use my TV Show to positively influence of the young generation.

QN: Ukiwa kama mwakilishi, kazi yako ni ipi hasa?

SPORAH: Kazi yangu ni kuwataarifu wana filamu wa Afrika Mashariki kuhusu fursa hii ya pekee ambayo ni fursa ya wao kuitangaza nchi na kutangaza filamu zao katika ngazi za juu. Na pia kualika viongozi wa serikali wa nchi hizo na balozi ili kushuhudia tuzo hizo zitakazofayika kwa siku tatu hapa nchini Uingereza.

QN: Muitikio wa wasanii wa nchi za Afrika Mashariki kutuma kazi zao ukoje?

SPORAH: Kusema ukweli muitikio sio mbaya, nchi za Afrika Mashariki zimejitokeza na kutuma kazi zao. Fingers cross filamu zao zifanikiwe kufikia vigezo vyote vinavyihitajika katika ZAFAA AWARDS 2013. (The Quality of the Movie eg: Picture & Sound)

QN: Umepokea filamu za kutosha kutoka Tanzania?

SPORAH: Sijui hata nianzie wapi kujibu hili swali maana ni aibu kwangu mimi. Mpaka sasa ZAFAA AWARDS 2013 haijapokea filamu yoyote kutoka nchi yaTanzania, ila bado sijafa moyo, hivyo bado nasubiri, nimekua nikisema labda kesho, labda kesho lakini naona siku zinazidi tu kusonga. Hopefully tutapata hata moja maana ninavyojisifiaga kwa watu na movie zetu za Bongo.!! hahaha..!
Nigeomba watunzi wa filamu za Tanzania wasiniangushe kwakweli. Waandaaji na hata waigizaji wajitokeze kuchukua fursa hii, na kutuma filamu zao. Hata kama hawatashinda au hawatafanikiwa kufikia kile kiwango ambacho kinahitajika katika ZAFAA AWARDS 2013.Uzuri wa ZAFAA AWARDS ni kwamba filamu yako kama haitafanikiwa kuingia katika mashindano, basi watakupa sababu za kwanini filamu hiyo haijafanikiwa kufikia kile kiwango chao ZAFAA AWARD.Which I believe Positive or negative feedback is a gift because you can learn from that, ili waki-record filamu nyingine waziweke kwenye standard ambayo inakubalika kimataifa.

QN: Ni vigezo gani vinavyotumika kuja kupata filamu bora?

SPORAH: Kigezo kikubwa ni picture quality and sound, then the Story, na je hiyo
filamu ilifanya vizuri kiasi gani locally (Original Country).

Filamu zinazohitajika ni za Kiingereza tu ama hata lugha nyingine pia?
Hapana, Filamu zinazohitajika sio lazima ziwe kwa Lugha ya Kiingereza. Lugha yoyote inakubalika ili mradi tu iwe na Subtitles ya kiingereza.

QN: Mwisho unatoa ushauri upi kwa waigizaji wa Tanzania utakaowasaidia kupata mafanikio kimataifa kuliko ilivyo sasa?

SPORAH: Kwanza kabisa, ni ku-jump into any kind of opportunity ambayo itakusaidia kuipa career yako exposure, maana hatujui lini au wapi mafanikio yatajitokeza. Wakati mwingine grabbing opportunities can seem scary but we’ll never know if we don’t go for it, I hate to think of the woulda,coulda, shoulda’s.
Also, Self Marketing as an artist is crucial to your success, as a movie star, a director or a producer, I think it is important to take all the opportunities that comes way, and thriving on the chances – and whatever happens next. Mungu ndiye anaejua, angalau unasema nilijaribu, kuliko “I WISH” (Laiti ningelijua)
Kuna msemo wa mtu maarufu anaejulikana kama Milton Berle unaosema “If opportunity doesn’t knock, build a door”
Watanzania tunatakiwa kujua kwamba opportunity is not a lengthy visitor, means that we need to learn to take advantage of an opportunity before it disappears;, Good things don’t wait around forever.

 
(Maoni ya Swahili worldplanet: Wadau wa filamu Tanzania jitokezeni ili kutuma kazi zenu maana nafasi kama hii ndiyo humtangaza zaidi muigizaji, director, producer n.k kimataifa. Tanzania tayari ni nchi inayozalisha filamu nyingi kuliko nchi yoyote ile ya Afrika mashariki hivyo kukosa kushiriki katika tuzo hizo kwa uzembe wetu wenyewe sio jambo zuri, tuchangamkie fursa, sio lazima tushinde ila kujitangaza zaidi kimataifa).

Pia najaribu kutafuta mawasiliano ya Sporah ili kuwaletea habari kamili ya namna ya kutuma kazi hizo.

                                                  Sporah Njau

No comments:

Post a Comment