Friday, June 28, 2013

MUIGIZAJI DIANA KIMARO BADO NI BIKIRA.

Diana Kimaro muigizaji wa Swahiliwood aliyejipatia umaarufu baada ya kuigiza filamu ya Family Disaster akiwa na Vicent Kigosi(Ray) na Elizabeth Michael(Lulu)  amesema kuwa yeye hana mpenzi wala boyfriend kwasasa na hataki kujihusisha na mapenzi kwa muda huu kwakuwa bado yeye ni mwanafunzi. Alisema kuwa yeye ni kama bikira vile na muda sahihi wa kuwa na mpenzi ukifika atachagua yule atakayekuwa sahihi kwa ajili ya maisha yake. Akiongea na filamucentral Diana alisema “Sijui kabisa mambo hayo na sijawahi kufanya upuuzi huo, ninaheshimu sana familia yangu baba yangu ni mkali sana hataki ujinga kwa hiyo si rahisi kudili na wanaume, mimi ni kama bikira vile, natoa nafasi kwa masomo kwanza sitaki kujichanganya na kuwa kituko mjini,”. Diana ameigiza filamu nyingi baadhi ni Poor Minds akiwa na Yusuph Mlela na Slim Omar, Kazi yangu akiwa na Yobnesh Yusuph(Batuli) na Danija akiwa na Jacob Stephen(JB), Adam Kumbiana na Mariam Ismail.

                              Diana Kimaro
         Diana na Lulu ambao walitamba na filamu ya Family Disaster


No comments:

Post a Comment