Wednesday, May 1, 2013

RAMMY GALIS ASEMA MIMI, IRENE UWOYA NA SLIM OMAR NI MOTO KATIKA FILAMU YA SNITCH.

Rammy Galis muigizaji anayekuja juu na ambaye pia alishacheza baadhi ya filamu na na marehemu Steven Kanumba huko nyuma anasema kuwa ujio wake mpya katika filamu ya Snitch Akiwa na Irene Uwoya na Slim Omar utakuwa moto wa kuotea mbali katika filamu hiyo iliyojaa visa vya ulaghai, usomi, ukatili, huzuni na mapenzi. Akizungumza na Swahiliworldplanet Galis alisema "Katika filamu hii Watanzania wategemee utofaut mkubwa sana kuanzia uchezaji wangu , story na wasanii wenzangu akiwemo Irene Uwoya na Slim Omary na wengine Wengi ambao wameonyesha uwezo wa Hali ya juu". Filamu hiyo inatengenezwa na kampuni ya Rakh Films Company huku muigizaji mkuu akiwa Rammy ambaye pia hivi karibuni alicheza filamu ya Malaika akiwa na Rose Ndauka na Seth Bosco.


No comments:

Post a Comment