Baada ya siku chache mtandao wa globalpublishers kuripoti kuwa Irene Uwoya anatembea na mwanamuziki Diamond kwa kufumwa wakiingia hoteli moja ya nyota tano na kutoka kesho yake mchana rais wa shirikisho la filamu Tanzania(TAFF) Saimoni Mwakifwamba amekaririwa na mtandao huo huo wa globalpublishers akisema kuwa Irene ni sikio la kufa hivyo halisikii dawa ikiwa ni siku chache tu tangu Uwoya kudaiwa kurudiana na mume wake Ndikumana. Mwakifwamba pia amesema Uwoya anajitia aibu pamoja na tasnia nzima ya filamu kwa kutokuwa kioo halisi cha jamii. “Uwoya anatakiwa
kujitambua kuwa ana nafasi gani katika jamii pia kwenye ndoa yake kwani
maisha anayoishi siyo mazuri na yanatia aibu familia na tasnia nzima ya
filamu hivyo abadilike,” alisema Mwakifwamba. Pia swahiliworldplanet ilijaribu kumtumia Uwoya ujumbe mfupi kuhusu sakata hilo yeye akiwa kama makamu mwenyekiti wa Bongomovies huku akikwaa skendo hiyo wakati klabu hiyo ilipoundwa waliapa kuwashughulikia watakaoichafua huku Uwoya mwenyewe akiwa tayari ameshaichafua kwa skendo yake hiyo hivyo watu kusubiri achukuliwe hatua na viongozi wenzake wa Bongomovie. Baadhi ya watu wake wa karibu wameiambia swahiliworldplanet kuwa Uwoya hataki kuulizwa kuhusu issue hiyo na akiulizwa hugeuka mbogo.
No comments:
Post a Comment