Friday, April 26, 2013

LADY JAYDEE AWEKA BAYANA HISTORIA YA MIZENGWE ANAYOFANYIWA NA CLOUDS FM.

Hivi karibuni mwanamuziki maarufu Afrika mashariki Lady Jaydee amekuwa akiituhumu waziwazi clouds fm kuwa imekuwa ikibana kupiga nyimbo zake na kuingilia katika mambo yake binafsi na hata biashara zake wakati alijua tofauti zao za kimtazamo zipo katika suala la muziki pekee. Watu wengi walionekana kumsapoti Lady Jaydee hasa katika mitandao ya kijamii kwa alichokisema na kukiandika katika kurasa zake katika mitandao ya kijamii na baada ya muda kidogo Selehe Ally mwandishi maarufu wa Globalpublishers aliandika makala iliyobeba kichwa cha habari kisemacho "Lady Jaydee mnafiki wa miaka 10 shujaa wa siku 30" na katika makala yake hiyo aliandika kuwa Lady Jay Dee amebebwa na Clouds kwa miaka 10 bila kusema chochote lakini hivi karibuni baada ya nyimbo zake kutokupigwa ndiyo akajitokeza kujifanya kuwa redio hiyo inapiga nyimbo za wasanii inaowataka wao na sio wasanii wa watu na wanaopendwa na watu. watu pia walikubaliana na makala ya Salehe kuwa Jaydee hakuungana na kina Sugu wakati wapo kwenye harakati kipindi kile kwa kuwa redio hiyo ilikuwa inambeba lakini sasa mambo yamemchachia ndiyo anajitia mwanaharakati wa muziki.

 Katika gazeti la leo la Dimba lilikuwa na makala iliyomhusu lady Jaydee na mwanamuziki huyo kuweka wazi zaidi kuwa watu wanamuona mnafiki wakidhani radio hiyo imeanza sasa wakati ilianza zamani kubana kupiga nyimbo zake sema alikuwa kimya kwa muda mrefu na alisema kuwa kuna mtangazaji mmoja aliwahi kukiri kuambiwa asilipige wimbo wake wa Malaika, akizungumza na mwandishi wa gazeti la Dimba Jaydee alisema "huwezi amini ndugu mwandishi ilifikia hatua viongozi wa radio walikataza watangazaji kupiga nyimbo zangu na wimbo wangu wa malaika kipindi unatoka mtangazaji mmoja alikiri kukatazwa kuupiga redioni kwenye kipindi chake".

Mwanamuziki huyo pia aliongeza kuwa wimbo wake wa Distance kutoka katika album yake ya Moto ulifanya vizuri sana mpaka kunyakua tuzo mbili za Chanel O. tuzo ya shirika la utangazaji la Uingereza(BBC) na pia ulichaguliwa kuingia kwenye tuzo za kora Afrika lakini haukufua dafu kwenye chati za redio Clouds bali ulikuwa unapigwa tu kwakuwa ulikuwa unapendwa na watu kwa muda huo "pamoja na hivyo wimbo huo haukufua dafu kwenye kituo cha redio Clouds kwani haukuwa kwenye chati yao na waliupiga tu kwasababu ulikuwa unapendwa na watu"

Jaydee aliongeza kuwa baada ya kutoa albamu ya" Shukrani" mwaka 2006 aliacha kutumbuiza katika Fiesta kwa kuwa walikuwa hawamlipi vizuri tofauti na gharama za maandalizi ya show husika "niliwaambia wanilipe shilingi laki 8 katika show hiyo ya mwisho, walilalamika na kunipa lakini toka hapo sikupewa tena dili hiyo kwakuwa nilionekana msanii ambaye wa ghali sana kuliko watu wengine hivyo ni bora waachane na mimi"

Amesema kuwa kilichommuudhi zaidi ni kuingiliwa mpaka katika biashara na maisha yake binafsi wakati suala lenyewe liko kimuziki. amesema pia kuwa tangu aanze kupiga show katika Band yake amekuwa hana wadhamini ila mungu amekuwa upande wake kwa kupata mafanikio hivyo watu wasimuone mnafiki wakijua suala hili limeanza leo wakati lilianza miaka kadhaa huko nyuma sema alikuwa kimya. Aliongeza kuwa aliingia katika ,muziki kama biashara na ndiyo maana amefanikiwa kwa juhudi zake.


No comments:

Post a Comment