Friday, April 26, 2013

DOTNATA ALISHWA SUMU YA KUMUUA TARATIBU !

Habari ni kuwa muigizaji wa filamu na mfanyabiashara maarufu Nchini Dotnata amewekewa sumu ya kumuua taratibu kwa kipindi cha miezi 8 sasa huku watu waliofanya hivyo wakiwa bado kujulikana. Muigizaji Amanda Poshy ameandika hiki kupitia facebook............................

"Kiukwelikati ya habari iliyonipa mshtuko mkubwa na iliyonifanya nikose nguvu ni kitendo cha mama yangu Dotnata kulishwa SUMU......nazungumzia sumu nikimaanisha sumu......mama yng hana matatizo na mtu...anacheka na kila mtu.....anampenda kila mtu.....hana ugomvi na mtu.....leo mtu unadiriki kumlisha sumu kweli?hayo ndio majibu ya dr baada ya mama yng kuumwa kwa muda mrf majibu yametoka amelishwa sumu ya kummaliza taratibu miezi nane iliyopita......nimeumia sana na aliyefanya kitendo hk atalaaniwa na Mwenyezi Mungu......inshaallah Utapona kwa uwezo wa Allah mama...pole sn...nipo pamoja nawe kwenye maumivu haya unayopitia"

Tunampa pole sana Dotnata na tunamuombea kwa Mungu apone haraka.

 

No comments:

Post a Comment