Sunday, January 27, 2013

NISHA ADAIWA KUTOKULALA USIKU NA MCHANA ILI AWE LADY GAGA WA BONGO

Styles za nywele alizoanza kutumia miezi ya hivi karibuni muigizaji maarufu na mwenye vituko vingi Nisha zimeanza kudiskasiwa/kujadiliwa na watu mbalimbali wakiwemo mashabiki wake kuwa anawaiga wasanii maarufu Lady Gaga na Nick Minaj ili aonekane tofauti na mastaa wenzake wa Bongo hivyo kujiongezea umaarufu. Watu hao wamekwenda mbali zaidi kwa kusema Nisha anaweza hata kuyanywea dawa makalio yake ili yatune kama ilivyo kwa Nick Minaji."si unaona nywele za Nisher kila siku ni za rangi tofauti, angalia matiti yake kama ya Nick Minaji na hata kope nafikiri bado makalio tu". Swahiliworldplanet kama kawaida lilimtafuta Nisha na kumuweka mtu kati na alikuwa na haya ya kusema "Nywele hizi nimenunua na sijachukua kwa Nicky wala lady gaga,,zinauzwa kama zinavyouzwa nyeusi,ila napenda crazy colours na ndio maana nazipenda,kila m2 ana role model wake,,mi wangu ni Nick minaj,,nampenda ila simuigi".

No comments:

Post a Comment