Pages

Wednesday, October 1, 2014

Meninah Utaishia Kula Makombo penzi La Diamond Platnumz: Hamisa Mobeto

Hamisa
Ni mtifuano kati ya Hamisa Mobeto na Meninah kisa penzi la Diamond Platnumz !....well, new celebrities' gossip zinasema kuwa Hamisa Mobeto amemrushia dongo  star mwenzake Meninah kisa kikidaiwa ni
wivu wa penzi la Diamond ambapo Hamisa Mobeto ambaye ni model maarufu nchini anayejikakamua pia katika tasnia ya filamu nchini siku za nyuma kudaiwa kutoka kimapenzi na Diamond na wawili hao wote kukanusha sasa ameamua kumwangalia Meninah kwa jicho angavu.

Kwasasa habari ambayo bado kupoa vizuri ni kuhusu Meninah kutoka kimapenzi na Diamond kwa siri huku mipango ya harusi ikidaiwa kufanyika kwa siri ingawa Meninah na Diamond wote wamekataa kutoka kimapenzi.

 Sasa basi chanzo kimoja rafiki wa Hamisa Mobeto ambacho kimesema  kuwa kinajuana sana na Meninah kikizungumza na Swahiliworldplanet  leo mchana kimesema kuwa Hamisa Mobeto ameshangazwa sana na habari za penzi la Diamond na Meninah kushupaliwa na kuandikwa sana na media ikiwemo mitandao ya kijamii wakati penzi lake na Diamond halikuzungumziwa sana kama ilivyo kwa Meninah huku Hamisa akionekana kuwa na wivu au kitu kilichojificha moyoni mwake.

"Hamisa Mobeto amechanganywa na habari za Meninah na Diamond kuwa wapenzi, u know Hamisa alishatoka na Diamond wakati Diamond anashuti moja ya video zake za nyuma, walishaachana but Hamisa wivu umemrudia ghafla baada ya kuona media zinaandika sana uhusiano wa Meninah na Diamond sijui hata what happened yeye anaumia zaidi kila siku anapoona habari za Meninah na Diamond kwenye media, nlikuwa nae juzi kwenye mgahawa flani akaona gazeti limeandika Meninah na Diamond kufunga ndoa basi aka-change mood ghafla nikashangaa, nlipomuuliza kulikoni akaishia kusema Meninah ataishia kula makombo penzi la Diamond, lazima kuna kitu tu kimejificha nakwambia" kilisema chanzo hicho chenye maneno mengi

Hata hivyo juhudi za kumsaka Hamisa Mobeto kuelezea madai hayo ya kumrushia dongo Meninah hazikuweza kuzaa matunda. Diamond juzi alimzawadia Wema Sepetu gari aina ya Nissan Murano katika birthday yake kama ishara ya kuonyesha kuwa bado wapo pamoja na wanapendana huku gossip za kutoka na Meninah zikiendelea kama kawaida.

                                            Meninah na Diamond
Like our Facebook page Swahili World Planet for more updates about Tanzanian movie stars' latest gossips, news, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news.

No comments:

Post a Comment