Cloud |
Kwa ,mujibu wa Didas Fashions ambaye ndiye mtengenezaji wa filamu hiyo ya Mateso Yangu Ughaibuni chaguo la kwanza la filamu hiyo alikuwa ni Frank Mwikongi na walizungumza mwanzo na kuafikiana Frank alipwe mil.2 kama gharama za kucgheza movie hiyo pekee lakini baadaye Cloud akaingia kati na kutaka yeye hiyo nafasi huku akidaiwa kumwambia Didasfacions kuwa Frank hawezi kuigiza wala kuongoza filamu(Ukweli ni kuwa Frank ana kipaji kikubwa cha kuigiza pengine kumzidi Cloud) kwa hiyo apewe yeye kazi ataifanya hata bure. Soma alichoandika Didas upate undani zaidi.............
"Jamani mnamuona huyu kaka hapa?(picha ya Frank) Huyu kaka anaitwa Frank kwa wale msiomjua. Huyu kaka ndio alikuwa aje UK kucheza movie ya MATESO YANGU UGHAIBUNI. Na tulisha kubaliana hadi bei maskini na kila kitu kilikuwa poa. Mara ghafla nikapokea simu ya kinafki, na wakati huo mie nilikuwa sijui lolote kuhusu bongo movie. Nikaambiwa huyu kaka ninae taka kumchukua hajui kucheza wala ku direct movie. Nika-pampiwa vibaya mnoo mpaka nikatia akili. Frank popote ulipo naomba unisamehe najua ulikuwa tayari umekuwa na tamaa ya safari ya kuja ulaya, ila waziba rizki wakafanya yao. Wacha naishi hapo. Hii ni intro tu. Hadithi kamili inakuja. Kaeni na ndimu zenu"
Baada ya muda kidogo tena Didasfacions akafunguka tena Instagram kwa kuandika........
"Haya uliniita mimi tapeli tena mdhulumati, nimekudhulumu million 8 za kuja kucheza movie, ukaenda mpaka kwenye magazeti kusema, nikapigiwa na wenye magazeti, nikawapa ukweli na ushahidi. Tena huu ni mfano tu, ninazo nyingi na za aibu, na bado naendelea. Frank aliniomba nimlipe Tsh 2 million kucheza hiyo movie, nikakubali, wewe ukasema kila kitu utafanya bure ila nikisha uza movie nikufikirie, sasa leo umemfanya @stevenyerere2 kajiuzulu eti kisa kanisaidia uzinduzi, na hela ya PSPF tumekula, huu ni mfano nakuja kumwaga mengi. Ulijitolea kila kitu bure uje ulaya, leo umenipaka mavi dunia nzima mimi tapeli, unawafanyia fitna watu wote wanao kaa karibu na mimi. Hii ni haki? Sawa mimi tapeli dhulumati, zote ni njia za kutafuta riziki. Tutafika hata mahakamani. Bado na rudi na mazito zaidi. Ongezeni ndimu"
Itaendelea kadri Didasfacions atakavyofunguka............ but moja ya mawasiliano ya Didasfacion na Cloud hayo hapo chini
Filamu ya Mateso Yangu Ughaibuni ilichezwa na Cloud, Monalisa, Riyama Ally na Wastara na ilizinduliwa hivi karibuni viwanja vya Leaders, Dar es salaam.
Frank
Haifai kuumbuana,tafadhali msitiri mwenzako usitoe siri zake nawe M/Mungu atakusitiri aibu zako siku ya Kiama. Tafadhali sana.
ReplyDelete