Pages

Friday, October 3, 2014

Esha Buheti: Nimejitoa Rasmi Kundi La Bongo Movie Unity, Kumejaa Fitna Na Majungu Na Halina Umuhimu Wowote.

Esha Buheti
"Naomba nitangaze rasmi kuanzia Leo mimiI ESHA SALIM BUHETI SIO MWANACHAMA WA BONGO MOVIE UNITY...
Kiukweli sijafaidika na chochote katika chama hiki zaidi ya kuwanufaisha wengine kupitia uanachama wetuu..... Ndani ya chama kuna makundi ambayo yamekaa Kazi kudidimiza wenzaooo thamanii yangu inaonekanaga ukitokea Msiba au ugonjwaa..... Kumejaa chuki fitna majunguuu halafu mbaya unaecheka nae ndo anaekumalizaa watu hawana hofu ya Mungu Kabisa..... Kuanziaa Leo mimi ni msanii wa kawaida kabisa kukitokea kitu nitajumuika kama msanii tuuu na hata nikifa leo najua sitakosa wakunizika!!!!" ameandika star huyo wa filamu nchini kupitia Instagram

Kundi la Bongo movie Unity ni sehemu ya kikundi kidogo tu katika tasnia ya filamu nchini wasanii wa kundi la Bongo movie unity wengi ni wale wenye majina huku wasanii wengi wakiwemo wale wachanga kuweka nguvu na matumaini yao katika Shirikisho la Filamu Tanzania(TAFF) ambalo ndio kubwa na chombo mama cha tasnia ya filamu nchini, mikakati yake ni kupigania maslahi ya wasanii wote na tasnia ya filamu nchini kwa ujumla, TAFF inaundwa na vyama mbalimbali vya wasanii wa filamu nchini lakini kundi la Bongo movie unity inadaiwa sio mwanachama sababu zikidaiwa ni kujiona ni maarufu na kila kitu huku wakiishia. Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania ni Simon Mwakifwamba huku aliyekuwa mwenyekiti wa kundi au club ya Bongo Movie Unity Steve Nyerere akijiuzulu hivi karibuni kwa madai ya kula pesa za kundi hilo kinyume na taratibu

No comments:

Post a Comment