Thursday, August 7, 2014

Diamond Amchefua Wema Sepetu, Mama Wema Na Mama Diamond Wafunguka.

Diamond Platnumz anadaiwa kumchefua mpenzi wake Wema Sepetu baada ya kutoa kauli kuwa hana mpango wa kuoa karibuni sababu anaweza kushuka kimuziki kama baadhi ya wasanii wenzake. Kwa mujibu wa mtu wa karibu wa mastaa hao, Wema hakufurahishwa na habari hiyo kwa sababu anajua yeye ndiye mke mtarajiwa wa Diamond.

Ilidaiwa kwamba, Wema alijikuta akipoteza ile furaha ya kwamba wawili hao wangefunga ndoa mwezi huu (Agosti) kama ilivyotabiriwa na mnajimu maarufu Bongo, Maalim Hassan Yahya Hussein.
“Baada ya kauli hiyo ya Diamond na kutotimia kwa utabiri wa Maalim Hassan kwa sababu hakuna hata dalili za maandalizi ya tukio hilo muhimu kwenye maisha ya mwanadamu, Wema ameanza kukata tamaa, lakini amesema hawezi kulazimisha ndoa kwa mwanaume kwa kuwa si utamaduni wa wanawake wa Kitanzania wala Kiafrika.
“Unajua Kibongobongo au hata Kiafrika hai-sound vizuri na pengine haiwezekani kwa mwanamke kulazimisha kuolewa kama mwanaume hataki. Hicho ndicho kilichomtibua Madam (Wema) baada ya kusoma alichokisema Diamond,” kilisema chanzo hicho kikizungumza na Globalpublishers na kuongeza:
“Wema amehisi yeye ni girl lover (mpenzi) tu kwa Diamond na si wife material (mke mwema) kwa hiyo  anawaza sana kuhusiana na ishu hiyo japo mahaba niue kati yao yanaendelea, lakini anafikiria kuchukua uamuzi mzito.”

Wema alipotafutwa alisema
“Mimi naamini sana mambo ya utabiri, lakini siumizi kichwa na suala la kuolewa na Diamond na kamwe siwezi kumlazimisha anioe.
“Kikubwa katika mapenzi ni upendo wa kweli ambao ananionesha bila kipimo. Wala sina papara, hata kama mtabiri kasema ndoa yetu ni lazima ifungwe mwaka unaogawanyika kwa mbili kwa maana ya mwaka 2016 kama itashindikana mwezi huu, hilo kwangu si tatizo la kunifanya nililie kuolewa na Chibu (Diamond).
“Ninachojua mimi Mungu ndiye anapanga yote na kama ndoa ipo ipo tu maana kuna watu wapo kwenye ndoa na hawana upendo wa kweli kama tulionano sisi,” alisema Wema.
MAMA WEMA ANASEMAJE?
 Mama yake Wema, Mariam Sepetu alipoulizwa alisema .....
“Mimi niseme nini? Sina la kusema kuhusu Wema. Mambo yake ni yake mwenyewe na huyo Diamond wake. Kwanza kwa nini mnipigie mimi, si mumtafute yeye mwenyewe?” alisema mama huyo kwa sauti ya utulivu.
MAMA DIAMOND AFUATA NYAYO
Katika hali ya kushangaza, mama Diamond, Sanura Kasim ‘Sandra’ ameonekana kunawa mikono kwa kauli aliyowahi kuitoa siku za nyuma kuhusu mtoto wake na masuala ya kutooa au kuoa.
"Nasibu ni mtu mzima sasa, siwezi kumpangia lolote kuhusu kuoa au kutooa. Wakati ukifika, anaweza kusema lolote ambalo ataliona ni zuri katika maisha yake.”
‘Diamond Platnumz’ akiwa na Bi mkubwa wake, Sanura Kasim ‘Sandra’.

No comments:

Post a Comment