Pages

Saturday, July 12, 2014

Wema Sepetu Ni Mnafiki: Kajala, Wema Ajibu Mapigo

Kajala
Star wa filamu nchini Kajala Masanja ameamua kumrarua Wema Sepetu kwa kusema ni mnafiki licha ya majuzi tu kusuluhishwa na kuondoa tofauti zao ila Wema anaonekana bado kuwa na kinyongo na Kajala. Kajala aliyasema hayo alipoulizwa na Globalpublishers ni kwanini hakuhudhuria birthday ya mama Diamond ambapo ni mkwe wa Wema Sepetu wakati mashost wengi wa Wema na mastaa walihudhuria. Kajala alisema Wema hakumualika licha ya yeye kumaliza tofauti zao na kujihisi hana tatizo kabisa na Wema.


"Wema ni mnafiki kabisa. Upatanisho wetu ni wa uongo. Mimi moyoni nimeondoa kinyongo lakini mwenzangu naona kama bado ana donge moyoni." alisema Kajala 

Aliongeza kwa kusema "Tunakubaliana kuwa kitu kimoja lakini mwenzangu anaonekana ana kinyongo. Hebu angalia, anawezaje kuacha kunialika kwenye shughuli muhimu kama ile kama kweli tumepatana? Mbona amealika watu wengi lakini mimi ameniacha? Wema aache unafiki bwana"
Wema na Kajala
Kajala alimshangaa zaidi Wema kwa kusema "Mbaya zaidi, hivi juzi tu ameweka picha ya msichana mmoja anayekaa China, huyu mdada anaitwa Sabrina, niliwahi kugomabana naye, lakini yeye amemuweka Instagram na kumwandikia maneno kibao ya kumsifia akim-wish happy birthday, hapo si kama ananisimanga? Wema si mkweli"

Wema Sepetu alipoulizwa kwanini hakumualika Kajala alisema "Ukiniuliza kuhusu Kajala kutokuwepo hapa, kwa kweli utakuwa kama unanichanganya tu maana leo sijashika simu muda mrefu sana.
“Hata ujio wangu hapa nilikurupushwa, ndiyo maana sijakumbuka kumuita Kajala, lakini tuko vizuri na mara ya mwisho tumeongea jana (Jumapili) usiku tu,” alisema Wema.

Wema
Like our Facebook page Swahili World Planet for more updates about Tanzanian movie stars' latest gossips, news, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news.

No comments:

Post a Comment