Pages

Thursday, July 10, 2014

Ray, JB Na Cloud Wasanii Wakubwa Wanaokwamisha Maendeleo Ya Tasnia Ya Filamu Nchini !

Cloud, Ray na JB
Mara nyingi nikiona mawazo mazuri ya wadau wa filamu kuhusu maendeleo ya tasnia hii huwa sisiti kuyachukuwa na kuyaweka kwenye blog. hicho hapo chini ndicho kilichoandikwa na Mkombozi wa wanafilamu 
 "HABARI NA POLENI NA MAJUKUMU YA KUTWA NZIMA.......
Ndugu zangu kama kuna jambo linaloyafanya matatizo ya wanafilamu yaonekane ni kansa na haiwezi kutibikasa basi ni damu ya kubaguana ambayo imeendelea kuwavaa kila kukicha.
Siku za awali kabisa kumbukumbu zangu zinanionyesha kuwa dhamira ya kuanzisha vyama ilitoka kwa wasanii wenyewe na hasa wasanii wenye majina makubwa.

Lakini jambo la kushangaza leo vyama vimesimama walau kwa asilimia arobaini ama zaidi lakini wasaanii hawa 
niliowaita wakubwa wote wamejitenga na hivi vyama kwa sababu zinazoonekana kukosa uzito ama mantik kutokana na kukinzana na tafsiri ya vyama.
Hadi hivi leo kuna orodha ndefu sana ya wasanii hawa wakubwa waliogoma kuungana na wasanii wengine na hasa waliojazana kwenye vyama hivyo kuweka msukumo wao ili kuhakikisha sekta ya filamu inapata mafanikio bila ya kuwa na msaada wowote kutoka kwa wasanii hao.
Ilihali mabadiliko yanayokusudiwa endapo yatapatikana hayatabagua mtu kwa namna yoyote ile na yawezekana hao waliosusia kufanya harakati ndiyo watakaokuwa wa kwanza kunufaika na hizo harakati.
katika hili yapo maswali mengi ya kujiuliza .

Je waliosusia wanajuwa wanachokifanya au wanatenda kwa matashi ya kundi ?
Lakini je hali ya sasa ya tasnia wadhika nayo au hawajaridhika nayo lakini
wanavumilia kwa sababu mke wamemzoweya na hawajui tabia za mke mpya ?
Pamoja na matatizo wanayoweza kudai kuwa ndiyo yanayosababisha kutojiunga na wenzao lakini yanafanana na umuhiomu wa jambo lenyewe?

Haya yote ukijiuliza wewe ambaye unakataa kutengeneza umoja na wengine kwa sababu ambazo unazijuwa mwenyewe utagundua kinachokusukuma kuyafanya hayo ni dhambi tu ya kuwabagua wenzio na hofu ya kujitawala ambayo kama kuitoa ni siku moja tu kama mwana adamu anavyozaliwa.
Tuache chuki majungu na fitina sisi sote ni mwili mmoja laiti kama wewe unayekiona leo umeyafikia malengo yako na hutaki na wenzi wayafikie ya kwao.
Je na wewe waliokutangulia wangeyafanya haya ungekuwa mgeni wa nani?
TUNAHITAJI WASANII WANAOWEZA KUONEKANA KAMA MWILI MMOJA NA SI WANAOBAGUANA KWA MAMBO YA KIPUUZI TU?
HAWA(aliweka picha za JB, Ray na Cloud)  NI MIONGONI MWA WASANII WALIOGOMEA KUJIUNGA NA VYAMA
TUAMBIZANE TU HATA WEWE AMBAYE UNAFAHAMU CHOCHOTE KUHUSIANA NA SABABU ZA WABABE HAWA TUNAO WAHESHIMU KUSUSIA KUUNGANISHA NGUVU ZAO KUTAFUTA UTATUZI WA MATATIZO YA SEKTA YA FILAMU."

SWP: Inasemekana baadhi ya wasanii wakubwa wa filamu nchini ndiyo wanazuia maendeleo ya kweli katika tasnia ya filamu nchini kwa kujionja ni mastaa na kujiweka katika kundi lao wanalojiita Bongo Movie Unity na hawataki kuungana na Shirikisho La Filamu Tanzania bila sababu zisizo na msingi huku ikidaiwa wengine wanahofia vyeo vyao kuonekana si kitu wakiungana na TAFF, but mimi nafikiri hakuna Tasnia ya filamu popote pale duniani iliyoendelea na kutambuliwa na serikali na pia kimataifa kama wanachokifanya Bongo Movie Unity, nafikiri bado wana upeo mdogo na wanahitaji kupewa elimu zaidi. Ustaa kitu gani ! walikuwepo mastaa, mliopo sasa mtachuja, damu changa yenye mapinduzi na ari ya kufanya filamu kimataifa itakuja. Bongo Movie Unity jitazameni Upya na kama TAFF wana dosari pia basi wote mkae chini muyamalize, muungane muwe sauti moja, ila kwa ufahamu wangu ni kuwa mlango wanaopitia TAFF ndiyo mlango ambao hata Hollywood na Bollywood walipitia kufika walipo sasa.
Like our Facebook page Swahili World Planet for more updates about Tanzanian movie stars' latest gossips, news, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news.

1 comment:

  1. Waigizaji wakubwa nchini India wamedumu kwa muda mrefu katika kilele cha mafanikio, hiyo iliwafanya wasanii wa nchi nyingine kufikiria njia mbada ya kufikia mafanikio zaidi ya waliofikia wao matokeo yake ni kama inavyoonekana hivi sasa, Korea inatamba na hakuna ubishi kwamba India wanakaa na kutazama kwa mbali sana hivi sasa...

    ReplyDelete