Wednesday, July 9, 2014

Bob Junior Ampa Tena Talaka Mke Wake Halima Ali !

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Bob Junior anadaiwa tena kuachana na mke wake Halima Ali ambaye ni actress wa filamu nchini Tanzania.
 wawili hao mwanzoni walidaiwa kuingia katika mgogoro na kupeana talaka baada ya Bob Junior kudaiwa kula mahaba na Ashley Toto ambaye ni muigizaji wa filamu za Kiswahili nchi za Scandinavia huku akiwa na asili ya Kenya ambapo wawili hao walikutana kikazi Bob Junior alipoenda Ujerumani kupiga show huku Ashley akiwa promota.

Sasa habari mpya zinasema kuwa Bob Junior amempa talaka mke wake ambaye walirudiana tena miezi michache iliyopita na kufunga ndoa upya na Bob Junior pia alipoulizwa na SWP alikiri kurudiana na Halima na kufunga nae ndoa upya. Inadaiwa kuwa Bob Junior amempa talaka tena mke wake ikidaiwa kuwa ndugu wa Bob Junior wanamuona Halima hana nyota nzuri kwasababu Bob Junior kama anashuka kimuziki tangu amuoe !. Wawili hao tayari wana mtoto mmoja

Tunamsaka Bob Junior na Halima na tutawaletea walichokisema.

Like our Facebook page Swahili World Planet for more updates about Tanzanian movie stars' latest gossips, news, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news.

No comments:

Post a Comment