Wednesday, July 9, 2014

Nilimtamani Kimapenzi Wema Sepetu: Martin Kadinda

Fashion designer wa Tanzania, Martin Kadinda amesema kabla hajawa manager wa Wema, awali aliwahi kumtamani kimapenzi Wema Sepetu, lakini alighairi baada ya kugundua ni mwanamke wa kudekadeka

Kadinda alitoa kauli hiyo wakati akizungumza na Globalpublishers kuhusu masuala mbalimbali yanayomhusu msichana huyo ambaye ana uhusiano wa kimapenzi na mkali wa Bongo Fleva, Diamond Platinumz.
Kuhusu maisha wanayoishi nyota hao wawili wapenzi, Kadinda alisema kwa jinsi wanavyoishi ni kama watu wanaoigiza, akitolea mfano wa kipindi walichorudiana wakiwa nchini China, ambako wenyewe walisema wanaigiza filamu wakati ndiyo kwanza walikuwa wanarejesha penzi lao lililovunjika mara ya kwanza.

Like our Facebook page Swahili World Planet for more updates about Tanzanian movie stars' latest gossips, news, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news.

No comments:

Post a Comment