Pages

Saturday, June 28, 2014

Kutana Na Annasiri Msangi, Star Wa Filamu Za Ndoa Yangu Na Hukumu Ya Ndoa Yangu.

Annasiri
Annasiri Msangi ni mmoja wa waigizaji wa kike nchini wanaofanya vizuri kwasasa hasa katika kuigiza nafasi za mama wa waigizaji wakuu. Kama ni mfuatiliaji wa filamu za kitanzania basi utakuwa ushamuona katika filamu mbalimbali zikiwemo ndoa yangu aliyoigiza na marehemu Steven Kanumba na Jackline Wolper, Hukumu Ya Ndoa Yangu aliyoigiza na JB na Shamsa Ford. Swahiliworldplanet ilipata nafasi ya kuzungumza mambo kadhaa na msanii huyu.

 Akihojiwa kuhusu lini alianza sanaa ya kuigiza alisema "Naitwa Annasiri Msangi, jina la sanaa naitwa Mama siri, nilianza kujifunza sanaa 1997 katika kundi linaloitwa Mwaloni sanaa Group, niliendelea kujifunza katika vikundi mbali mbali vya sanaa, nimecheza filamu nyingi nilizoshirikishwa, baadhi ni Tafrani, Macho Yangu, Jonhson, Kazi Yangu, Life To Life, Kashifa, My Intention, Deal Fake, Big Brother, The Grave, Dunia Ya Machozi, Pigo La Yatima, Shella, Ndoa Yangu, Hukumu Ya Ndoa Yangu, na filamu nilizo cheza ambazo zitaingia dukani muda si mrefu ni The stolen Dreams, Ndoa Ya Majini, Kinyongo, Jois, Kitoga, Malikia Adela, Mikono Salama, Mama Wa Marehemu, Chausiku"
Annasiri

Kuhusu mafanikio aliyoyapata mapaka sasa akiwa kama msanii alisema " kwasasa ninashukuru maana nimepata mafanikio mengi kupitia sanaa na pia mimi ni mjasiliamali'

Kila kazi haikosi changamoto zake ikiwemo sanaa, kuhusu hilo msanii huyo anayejipenda akizungumzia changamoto za kuwa mcheza filamu alisema "Changamoto ni nazopitia ukwli pale unapohitajika kwenda eneo la kazi au location unahitajika saa 12 asubuhi na kuambiwa shuuti inaanza saa 2 asubuhi matokeo yake shuting inaanza saa 9 jion, ukiulizwa anasubiriwa mtu mmoja tu hajafika location yaani inaumiza sana je sanaa yetu itapiga hatua kweli? Halafu hapo umesaini mkataba kuwa hii kazi itafanyika kwa siku 4 sasa kutokana na Pm au production meneja kutokuwa makini basi hiyo kazi utaifanya kwa siku 7 ukweli inaumiza tubadilike, tuiheshimu sanaa ni kazi sio tu chombo cha burudani jamani"

Like our Facebook page Swahili World Planet for more updates about Tanzanian movie stars' latest gossips, news, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news

No comments:

Post a Comment