Thursday, May 22, 2014

Nisha Awapiga Kikumbo Gazeti La Sani Kuhusu Filamu Ya Zena Na Betina.

Habari mpya ni kuwa uongozi wa gazeti la Sani umemruhusu na kumpa baraka zote star wa filamu nchini Salma Jabu Nisha kuingiza sokoni filamu yake mpya ya ZENA NA BETINA baada ya hapa awali kuingaia katika mkorogano kwa madai nisha amaetumia majina ya katuni zao katika gazeti hilo. Hata hivyo Sani wamebaini kuwa story ya filamu hiyo ni tofauti kabisa na yao.

Hivi majuzi ilidaiwa kuwa Sani wamemburuza Nisha kotini na kumtaka atoe fidia ya mil.100 kisa kutumia majina hayo kabla ya kukaa chini na kuyamaliza. Kwa hiyo filamu hiyo ambayo tayari inasubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki itaingia sokoni tarehe 29 mwezi huu kama kawaida. hakikisha unanunua nakala yako halisi.

No comments:

Post a Comment