Thursday, May 22, 2014

VAD Waibiwa Camera Kiutatanishi, Waahidi Zawadi Nono Kwa Atakayetoa Taarifa Ilipo.

Camera iliyoibiwa
Wasanii wa kundi la Voice Of Africa In Denmark(VAD) ambao wanajishughulisha na sanaa ikiwemo kutengeneza filamu kwa kiswahili nchini Denmrk wamepata masahibu ya kuibiwa moja ya camera zao muhimu. Tukio hilo limetokea baada ya cameraman wao kuchukuwa camera hiyo aina ya canon inayoonekana pichani ili kwenda kushuti scene fupi uwanja wa ndege lakini cameraman huyo kumlazimu kupitia nayo nyumbani ili kusubiri kukutana na director na ndipo ikakwapuliwa na watu ambao hawajajulikana mpaka sasa. Kwa mujibu wa mmoja wa viongozi wa VAD mwizi huyo atawatia hasara kwakuwa katika camera kulikuwa na memory yenye vipande vya filamu yao mpya hivyo halikuwa tukio la kiungwana hata kidogo.

Mmoja wa viongozi wa VAD akizungumza na SWP amesema kuwa tayari wameripoti tukio hilo polisi na uchunguzi unaendelea lakini pia watatoa zawadi nono  kwa mtu yeyote atakayewapa taarifa au tetesi za kamera hiyo ilipo. Kwa hiyo kama unajua ilipowasiliana na VAD hapa HAPA

No comments:

Post a Comment