Wednesday, April 30, 2014

Hashim Kambi Amjibu JB Baada Ya Kusema Haoni Umuhimu Wa Kusomea Filamu Kwa Madai Tayari Anakubalika !

Hashim Kambi
Ramsey Hashim "Hashim Kambi" ambaye ni star wa filamu aliyejizoelea umaarufu na pia kuigiza na waigizaji wakubwa wa Ghana kama Van Vicker na John Dumelo amesema kuwa kuna kila sababu ya wasanii wa Tanzania kuongeza elimu kuhusu filamu badala ya kutegemea vipaji pekee kwani nchi nyingine zilizopiga hatua kubwa katika fani hiyo wameweka kipaumbele katika  elimu ya filamu badala ya kutegemea vipaji pekee. "kipaji peke yake hakitoshi wenzetu wamefanikiwa kupiga hatua katika filamu kwasababu waliamua kwenda shule kuisomea hii fani......kwani kwa kiasi kikubwa kufanya filamu bila elimu kunachangia kudharaulika kwa filamu zetu" alisema star huyo ambaye hufanikiwa kuubeba uhalisia katika filamu nyingi anazoigiza kiasi cha kuwafunika waigizaji wakuu wa filamu hizo mara kwa mara wakati akizungumza na Sani


Alichokisema Hashim Kambi kinadaiwa kuwa kama jibu kwa mwigizaji mwenzake Jacob Stephen(JB) ambaye wiki iliyopita alikaririwa akisema kwa umri alionao hawezi kwenda kusomea filamu kwasababu tayari anakubalika kwa hiyo suala la kusoma anawaachia vijana wakasome na baada ya kurudi wawape uzoefu hao vijana."Kwa umri huu eti mtu anipeleke nikasomee kuigiza wakati uwezo wangu wa kuigiza unakubalika na watazamaji wangu, hapana siwezi kufanya hivyo, bali sasa vijana ndio waende wakasome waje tuwapokee na kuwapa uzoefu" alisema JB wakati akizungumza na Filamucentral

Jb
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx

Filamu kali ya SIO SAWA inaingia sokoni Ijumaa hii April 2014 hakikisha unanunua nakala yako halisi.
Follow us on twitter Swahili World Planet  and Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies SWP for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities, features, beauty, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news, life styles news and 

No comments:

Post a Comment