Wednesday, April 30, 2014

Ray Adai Kuwa Na Pesa Na Mali Nyingi Kuliko Msanii yeyote Yule, Awapasha Wabaya Wake.

Ray
Star wa filamu nchini Vicent Kigosi "Ray" amesema kuwa yeye ana pesa na mali nyingi na hakuna msanii yeyote wa filamu anayemfikia sema hapendi tu kujitangaza kama baadhi ya mastaa wenzake akidai ni ulimbukeni. "hakuna msanii anayenizidi uwezo kuanzia mali na hata fedha niko mbali sana mimi, hata gari ninalotembelea hakuna msanii aliyenalo kama ingekuwa ni mtu wa kujisifusifu na kutafuta sifa za kijinga jamii ingejua" alisema star huyo wa filamu za Oprah, Sobbing Sound, Hard Price na Handsome Wa Kijiji akizungumza na gazeti moja.


Ray vile vile aliamua kurusha kombora kwa wabaya wake wasiopenda maendeleo yake kwa kusema "wanaongea sana majungu,  fitina na vitu ambavyo havipo kuhusu mimi, mimi ni jembe, kwanini wasiangalie maisha yao? leo msanii unateta nae dakika hiyo hiyo anageuza maneno hayo kuwa majungu, acha nikae peke yangu nifanye issue zangu"

xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx

Filamu kali ya SIO SAWA inaingia sokoni Ijumaa hii April 2014 hakikisha unanunua nakala yako halisi.
Follow us on twitter Swahili World Planet  and Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies SWP for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities, features, beauty, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news, life styles news and 

No comments:

Post a Comment