|
Wema Sepetu |
Hivi juzi kati Wema Sepetu alialikwa kama mgeni rasmi katika hafla ya chuo cha TFCT cha mafunzo ya filamu kinachomilikiwa na Emmanuel Myamba "Pastor Myamba" ambaye pia ni star wa filamu nchini. Wema alialikwa kwa shinikizo la wanafunzi wa chuo hicho sambamba na Jokate Mwegelo. Wema aliombwa mwanzoni kuhudhuria tukio hilo na kukubali hata hivyo Wema alipopigiwa simu hatua za mwisho alisema hataweza kufika kwasababu amepata msiba wa shangazi yake. Lakini ikabainika kuwa Wema alimdanganya Myamba kwani hakukuwa na msiba wowote wa shangazi yake kwa mujibu wa chanzo kilicho karibu na Wema kilichozungumza na
Globalpublishers, ambapo kilisema kuwa kama kungekuwa na tukio la msiba wangejua tu kwani Wema huwa hawafichi na siku hiyo walikuwa na ratiba ya kwenda kwenye tukio moja la starehe ambalo ratiba yake haikubadilika.
Baada ya tukio la Wema kuikaushia hafla hiyo ilibidi waandaaji wawaombe radhi wageni waalikwa wakiwemo waandishi wa habari, Myamba alipotafutwa na GPL na kuulizwa kuhusu tukio hilo alikiri na kusema amesikitishwa sana na Wema kwa alivyofanya kwani alialikwa kutokana na heshima aliyonayo.
"Nimemshangaa sana lakini mbona mwenzake Jokate alikuja, ni kwasababu anajitambua na ni professional alisema Myamba ambaye alipata umaarufu kwa kuigiza filamu nyingi na marehemu Steven Kanumba akicheza nafasi kama pastor.
Myamba
Follow us on twitter Swahili World Planet and Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies SWP
for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities,
features, beauty, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and
Nollywood news, life styles news and more
No comments:
Post a Comment