Friday, March 7, 2014

Photos: Niler Bernad Kuiwakilisha Tanzania Katika Top Model Of The World 2014 Nchini Misri.

Niler Bernad
Mwanamitindo Niler Bernad anatarajiwa kuiwakilisha Tanzania katika mashindano ya Top Model Of The World yatakayofanyika nchini Misri mwishoni mwa mwezi huu wa tatu. Akizungumza na Swahiliworldplanet Niler alisema "I won the tittle ya Tanzania Top Model 2013 ambayo ilikuwa chini ya Tanzania Top Model Agency ,hivyo mwishoni mwa mwezi wa 3 naenda nchini Misri(elgouna) kuiwakilisha Tanzania katika mashindano ya TOP MODEL OF THE WORLD yanayofanyika kwa mara ya 21 mwaka huu, Tanzania ikiwa ni moja ya nchi 6 Africa zilizobahatika kupata nafasi ya kupeleka washiriki, nchi nyingine 44 zikiwa ni kutoka mataifa mbalimbali"
Niler akiwa katika pozi.
Kuhusu umri wake na lini alianza modelling Niler mwenye sifa za kuwa mwanamitindo wa kimataifa alisema "Nina miaka 21, nilianza modelling kwa mara ya kwanza mwaka jana September na nilishafanya shows mbili ya Mini Fashion Week Zanzbar na Zanzibar Fashion Week iliyofanyika visiwani Zanzibar ikisimamiwa na zanzibar fashion" 

Niler
 Niler alimalizia kwa kusema "Nikaingia kwenye mashindano hayo na baadaye ndio nikawa mshindi na safari yangu ikawa serious kuanzia hapo but it is something that i have always wanted to do.

                                                  We wish you all the best


Make up :        Upendo Shuma
Photographer:   Albert Manifester






Follow us on twitter Swahili World Planet  and Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies SWP for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities, features, beauty, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news, life styles news and more

No comments:

Post a Comment