Single Mtambalike "Richie" |
Kwa mujibu wa bongomovies Richie aliyazungumza hayo jana wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kusaka vipaji nchini toka kampuni ya filamu ya Proin Promotions. Richie alisema kuwa vyombo vingi vya habari vinapenda kuwafuatilia sana waigizaji wenye skendo hasa za mapenzi kwani habari hizo ndio zinauza sana na kupendwa kusomwa na watu wengi na kuacha kuandika mambo ya maana yatakayoijenga tasnia ya filamu nchini.
Richie alitilia mkazo kwa waandishi wa magaezti, blogs na vyombo vingine vya habari kuwa kama kweli wanataka kukuza Sanaa hii ya filamu nchini, basi hawana budi kuepukana na kasumba hiyo na kuandika mambo yenye maana.
Richie atakuwa mmoja wa majaji katika shindano hilo la kusaka vipaji nchini litakalojulikana kama Tanzania Movie Talent.
No comments:
Post a Comment