Kajala |
Vyanzo hivyo vinadai kuwa, kigogo huyo wa Ikulu ni yule Clement ambaye amewahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Wema Sepetu.
"Mmeisikia hii? Kajala amenunuliwa gari na Kile (Clement), lina thamani ya shilingi milioni kumi na moja, Wema alie tu nakwambia. We ukisema cha nini wenzako wanajiuliza watakipata lini?"
Brevis aina ya gari analodaiwa kununuliwa Kajala |
Kajala alipotafutwa na Globalpublishers kupitia gazeti lake la Risasi Jumamosi mazungumzo yao yalikuwa hivi..........
Risasi: Mambo Kajala?
Kajala: Poa tu, mambo?
Risasi: Mambo poa. Eti, namba za gari lako Toyota Brevis ni ngapi?
Kajala: Mh! Yaani hata mimi mwenyewe sizijui, sijazishika kabisa.
Risasi: Sasa, kuna habari kwamba hilo gari umenunuliwa na Clement, yule aliyekuwa na Wema zamani. Kuna ukweli wowote?
Kajala: Mh! Hizo habari si za kweli. Wapo watu wanajiita Team Wema ndiyo wameamua kunipakazia hivyo, wameandika hadi kwenye Instagram, lakini siyo kweli kabisa.
“Mimi nimelinunua hili gari kwa mtu. Aliniuzia kwa shilingi milioni kumi na moja (11,000,000). Sijahongwa wala sijanunuliwa. Kuna watu wanataka kunichafua tu.
Kuhusu kusambaratika kwa urafiki wao, awali Kajala hakutaka kulizungumzia suala hilo lakini alipobanwa alidai hana tatizo na Wema na kwamba kwa sasa yuko busy kutengeneza filamu zake. Kwa upande wa Wema Sepetu alipopigiwa simu hakupokea lakini siku za nyuma aliwahi kuanika kwamba haamini kama Kajala anaweza kutembea na Clement. Hapo ni wakati ule wakiwa mashoga wa kutupwa.
No comments:
Post a Comment