Saturday, March 29, 2014

Dr.Cheni Ndie Aliyenishawishi Kuingia kwenye Uigizaji: Philimon Lutwaza

Philimon Lutwaza sio jina geni kwasasa katika tasnia ya filamu Tanzania, tayari amefanikiwa kujiweka kwenye kundi la mastaa wa filamu. Lutwaza alianza sanaa muda mrefu huku muonekano wake ukidaiwa kushabihiana kwa asilimia kadhaa na marehemu Steven Kanumba, pia amecheza kama mmoja wa wahusika wakuu katika filamu ya After Death iliyoandaliwa mahususi kwa ajili ya kumuenzi Kanumba. Kuhusu ni lini alianza kuigiza akichonga na Swahiliworldplanet Lutwaza alisema "Nilianza sanaa mwaka 2001 katika kundi la Fukuto Professional Art Group na aliyenishawishi ni Dr.Cheni, Baadhi ya filamu nilizocheza Bad Nigh(2008), Branch Of Love(2009), Beautiful(2010) ,tamthilia ni Jasmin(2008), Millosis(2010), Red Apple(2011)"
Alipoulizwa aliipataje nafasi ya kucheza kwenye filamu ya After Death na mapokeo yake ilikuwaje alisema " nafasi ya After Death ilikuwa inahitaji mtu kama mimi ndipo producer &director waliponitafuta, kuhusu mapokeo ya After Death nashukuru Mungu ni mazuri kupitia maoni mbali mbali ninayoyapokea"

Kuhusu kama ameshaoa au bado na je hapati usumbufu yeye akiwa kama mmoja wa waigizaji wa kiume watanashati kwenye industry "Lutwaza alimalizia kwa kusema "sijaoa na sipati usumbufu" 


Follow us on twitter Swahili World Planet  and Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies SWP for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities, features, beauty, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news, life styles news and more

No comments:

Post a Comment