Lucy Komba |
Lucy Komba akiwa hewani na mtangazaji wa Swahili Talk Radio Rehema Nkalami |
Hata hivyo baadaye Lucy akawa hewani na alipoelezwa kuhusu kumchana radioni Ashley Toto star huyo wa muda mrefu na mwenye uwezo wa kuuva uhusika katika filamu alisema"ha ha ha sijamponda nani kakwambia yeye mwenyewe? sijampoda ila aliniuliza niwashauri nini wasanii wa huku nikamwambia wafanye kazi siyo mtu anacheza scene moja anaanza kujitangazia ustar watu wanatakiwa waone nini msanii kafanya ndiyo wampe sifa hiyo ndo kazi ya sanaa lakini sijaponda yeyote wala sijataja jina la yeyote mbona wasanii wa hivyo wako wengi lakini nashangaa watu wanapenda umaarufu au wanapenda ugombana au kujibizana na mastar ili wawe mastar kupitia sisi kuna mwingine nae analalamika eti mimi nimemponda siyo huyo tu wanajoshtukia na kama wanahizo tabia kweli waache"
Lucy ambaye anasifika nchini Tanzania kwa kujipatia umaarufu kutokana na filamu zake na sio skendo kama baadhi ya mastaa wenzake walivyo alisema kuwa hata hamjui huyo Ashley "Ila huyo msanii mimi simjui wala sijawahi kuona kazi alizocheza na pia waache kujitangazia u-star. U-star unakuja wenyewe taratibu siyo wa kujilazimisha aache kelele afanye kazi watu waone, mastar wenyewe wamekaa kimya"
Star huyo wa filamu za Yolanda na Pretty Teacher alimalizia kwa kusema " halafu kawaida yangu huwa sipendi mabifu na watu ndo maana huwa nakaa kimya ila wakinichokoza nitaongea, ila watu wanataka nicharuke maana kila ninachofanya wanaanza maneno nikicharuka hawatanishika waambie. huwa sipendi upumbavu.....waandikie ninachoongea. nimefunga mdomo.kwa muda mrefu ila mbwa ukimzoea anakufuata mpaka masikitini sasa sitaki mazoea na mbwa"
No comments:
Post a Comment