Monday, March 31, 2014

Filamu Za Tanzania Zazitoa Filamu Za Nigeria Katika Soko La Afrika Mashariki Na Kati.

Baadhi ya wasanii wa filamu Tanzania wakiwa na Rais Kikwete akiwemo marehemu Steven Kanumba
Filamu za Tanzania zimefanikiwa kuzindoa sokoni filamu za Nigeria katika nchi za Afrika mashariki na kati tofauti na ilivyokuwa mwanzoni mwa miaka ya 2000 ambapo filamu nyingi za Nigeria zilionekana kutamba sokoni kwa kukosa mpinzani wa kweli Afrika mashariki na kati lakini Tanzania ikajitosa rasmi kwenye filamu na kutoa upinzani mkali kwa Nigeria ambapo sasa Nigeria tayari imeonekana kulipoteza soko la Afrika mashariki na kati. Vyanzo kutoka Burundi na Congo vikizungumza na Swahiliworldplanet vinasema kuwa asilimia kubwa ya watu wa nchi hizo hawazijui filamu za Nigeria bali wanazitambua na kuziangalia sana filamu za Tanzania na kuna vituo vya Tv ambavyo hurusha filamu za Tanzania kila siku kwa mujibu wa chanzo cha uhakika kutoka Burundi.
William Hatungimana ambaye ni ni mzaliwa wa Burundi na shabiki wa filamu za Tanzania ambaye hajawahi kufika Tanzania alipoulizwa kuhusu soko la filamu za Tanzania nchini Burundi alisema "zina hit na east Africa Tanzania ndio inaongoza kwa filamu na mara nyingi wachezaji(wasanii) wetu wanapenda wacheze pamoja na watu wa Tanzania maana wa Tz wako level zaid yetu"

Alipoulizwa tena je kati ya filamu za za Nigeria na Tanzania zipi zinapendwa zaidi nchini Burundi kwa kujiamini alijibu " kiukwel 90% hawazijui filamu za Nigeria but wanapenda za kitanzania because wanazielewa zaidi tena wanaelewa kiswahili, tena huku tuna Tv inaonyesha everyday filamu za huko Tanzania"

Chanzo kingine nacho kutoka nchini Congo kilichojitambulisha kwa jina Jovin kilisema kuwa Tanzania ipo juu kwenye filamu Afrika mashariki na kati kiasi kwamba filamu za Tanzania zinafanya vizuri nchini Congo kuliko za nchi yoyote ile ya Afrika ikiwemo Nigeria. "wee Tanzania tunawakubali mnafanya vizuri sana, Nigeria haina nafasi huku(Congo), wasanii wa filamu Tanzania wanajulikana sana huku"

Hata hivyo chanzo kimoja kutoka nchini Kenya kimesema kuwa wakenya sio wapenzi sana wa filamu za Kiswahili hasa wasomi wa vyuo vikuu pengine sababu ikiwa ni kushikilia sana kiingereza . Vilevile hivi karibuni muigizaji wa Ghana Majid Michael aliingia katika mtifuano na producers wa Ghana baada ya kusema kuwa Ghana hakuna tasnia ya filamu bali ipo nchini Nigeria hii inaonyesha kuwa mpinzani mkubwa wa filamu za Nigeria katika soko la Afrika ni Tanzani kwani Ghana wanabebwa na Nigeria huku nchi nyingine za Afrika zikisusua katika uzalishaji wa filamu licha ya baadhi kuzalisha filamu zenye ubora wa kimataifa ikiwemo Afrika kusini.

Miaka ya hivi karibuni wasanii wa filamu Tanzania wamekuwa wakipokelewa na maelfu ya mashabiki katika nchi za Afrika mashariki na kati kushinda hata viongozi wa kitaifa kuonyesha ni jinsi gani kazi zao zinapendwa, baadhi ya wasanii hao ni pamoja na marehemu Steven Kanumba, Jacob Stephen(JB), Vicent Kigosi(Ray), Irene Uwoya, Johari n.k

Maoni hayo ya watu wachache yanaweza kuwa chachu ya serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Shirikisho La Filamu Tanzania(TAFF) kufanya research zaidi ili kulijua vizuri soko la filamu za Tanzania katika nchi za Afrika katika wakati huu wa vuguvugu la kuifanya tasnia ya filamu nchini kuwa sector rasmi, Ambapo moja ya malengo makuu ni kuongeza ubora wa filamu za Tanzania na kuwa nchi namba moja Afrika katika tasnia ya filamu na pia kuingia soko la nje ya Afrika, kuongeza ajira, kuingiza fedha za kigeni kupitia filamu na kukua kwa pato la msanii mwaka hadi mwaka na kuitangaza utamaduni na nchi kimataifa kupitia sekta ya filamu. Hayo yatawezekana ikiwa wadau na wasanii watatilia mkazo elimu ya filamu, ubunifu, ushirikiano kwa wasanii wenyewe na serikali kutoa kipaumbele katika tasnia hii.
                                        Baadhi ya wasanii wa filamu nchini Tanzania


Follow us on twitter Swahili World Planet  and Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies SWP for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities, features, beauty, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news, life styles news and more

No comments:

Post a Comment