Monday, March 31, 2014

Baby Madaha Apanga Kumfumua Shilole.

Baby Madaha
Zile ngonjera za Baby Madaha na star mwenzake wa filamu na muziki pia Shilole bado zinaendelea safari hii Madaha akidaiwa kupanga kumfunza adabu Shilole kwa kumpa kipigo. Sababu za Madaha kudaiwa kutaka kumtia mikononi msanii mwenzake huyo ni kuwa Shilole amekuwa hampatilizi sana na kujibizana na Madaha kwenye media na amekuwa akiingia kwenye anga za Baby Madaha na kujifanya yupo juu zaidi yake. Chanzo kilicho karibu na Madaha kikichonga na Swahiliworldplanet kilisema " Baby madaha anapanga kumfumua Shilole coz ameona Shilole anampuuza,Shilole anaona yupo juu kisanaa kuliko Baby"


Baada ya kurushiwa news hizo na kuzinyaka tulimsaka Baby Madaha na kumweleza kuhusu madai ya kutaka kmshushia kipigo shilole hata hivyo Madaha alishia kuangua kicheko tu bila kuongeza neno lolote "ha ha ha haaaa" alianhua kicheko Baby Madaha.

Mastaa hao wawili wamekuwa katika tifu la kutafutana na kurushiana maneno ya shombo kwa muda mrefu sasa huku Baby Madaha akidaiwa kuwa chanzo kwa kumfuafuata Shilole.

Shilole
Follow us on twitter Swahili World Planet  and Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies SWP for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities, features, beauty, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news, life styles news and more

No comments:

Post a Comment