Wednesday, November 6, 2013

WASANII TUUNGANENI KWA DHATI ILI KUEPUKA KUNYONYWA NA WASAMBAZAJI: DUDE

Actor maarufu Swahiliwood Kulwa Kikumba(Dude) amesema kuwa licha ya tasnia ya filamu kukua nchini na kupokelewa vizuri na wanunuzi lakini bado wasanii hawanufaiki na filamu zao kutokana na kwamba wasambazaji wanawanyonya wasanii sana kwa kuwalipa pesa ndogo huku wasanii wenyewe wakiwa hawana umoja wa dhati ili kuwa na msimamo thabiti wa kukomesha hali hiyo. Akizungumza na Bongo5 Dude alisema "kuna baadhi ya watu na wadau wa filamu hawataipokea vizuri kauli yangu especially kwa wasanii wenzangu, nikiwemo mwenyewe nasema sisi hatujitambui kabisa, hivi inawezekana vipi wasanii wote tukatawaliwa na mtu mmoja kama vile mtu aliyeoa wake wengi wasio na maamuzi? ufanye filamu lazima upeleke kwa wasambazaji wahindi na wanatupeleka wanavyotaka"

Dude ambaye alijipatia umaarufu pia kupitia kipindi cha Bongo Dar es salaam aliongeza kwa kusema "tungekuwa na ushirikiano sisi wasanii tungefika mbali sana, kutokana na jinsi filamu zinavyolipa lakini kutokana na jinsi wasanii wachache wananufaika basi wanajisahau na kuwasahau wenzetu ambao wanalalamika kila siku. Nadhani kama tungeshirikiana wasanii wote tukawa tunauza filamu kwa bei za usawa kutokana na ubora na gharama ya filamu tungefika mbali sana"

                                                      Dude
Follow us on twitter Swahili World Planet  and Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies SWP for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities, features, beauty, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news.

No comments:

Post a Comment