Wednesday, November 6, 2013

LULU AKANUSHA HABARI KUWA AMECHUMBIWA.

Star mkubwa wa filamu Swahiliwood Elizabeth Michael(Lulu) amekanusha habari zilizoandikwa na gazeti la udaku "Filamu" kuwa amechumbiwa. Lulu alisema hajachumbiwa na haelewi habari hizo zimetoka wapi " mimi sijachumbiwa na hakuna mtu yeyote aliyenichumbia na kama ikatokea siku nikachumbiwa kila mtu atajua na mimi mwenyewe ndiye nitakayesema" alisema Lulu akizungumza katika kipindi cha XXL cha Clouds fm.

Star huyo aliyejipatia umaarufu tangu akiwa mdogo aliongeza kwa kusema "lakini sasa sijajua wao wamepata hiyo habari kutoka kwenye chanzo gani, by the way kumekuwa na habari kila kukicha kila mtu anayejisikia kuandika anaandika, anaamka anaandika kwa hiyo leo wameandika nimechumbiwa kesho wataandika nimeolewa, kwa hiyo inategemea na mood ambayo wao waliamka nayo kwamba leo Lulu tumchumbie, tumuozeshe, tumuachishe i don't know"

Lulu Alimalizia kwa kusema "kuchumbiwa, kuolewa, kuwa mke ni vitu ambavyo tumeumbiwa binadamu, vipo kama ukiwa mpango wa mwenyezi Mungu nitachumbiwa na nitaolewa"

                                                                    Lulu
Follow us on twitter Swahili World Planet  and Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies SWP for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities, features, beauty, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news.

No comments:

Post a Comment