Monday, September 30, 2013

BEHIND THE SCENES: AFRICAN BOY STARS LUCY KOMBA, ABOU HERMIS, JEAN CLAUD AND RASHEL SCHARP.

African Boy ni filamu mpya ya Kiswahili ambayo imewakutanisha waigizaji wa nchi mbalimbali akiwemo Lucy Komba ambaye ni star wa Swahiliwood, pia yumo Abou Hermis ambaye ameigiza kama mume wa Lucy Komba. Waigizaji wengine ni Jean Claud kutoka Congo ambaye kwasasa anaishi Denmark, Rashel Scharp kutoka Tanzania ambaye ni mwanamuziki wa nyimbo za injili lakini akiwa anaishi nchini Sweden na Fatma ambaye ni mtanzania. Sehemu kubwa ya filamu hiyo imemalizika kushutiwa kwasasa na filamu hiyo inatarajiwa kuanza kuingia sokoni mwezi wa kumi na moja(November) mwaka huu. Pia inatarajiwa kufika Tanzania na Afrika mashariki kwa ujumla. Filamu hii imetengenezwa na Twaleb Entertainment. Angalia baadhi ya picha za behind the scenes.....................

                                       Lucy Komba
Abou Hermis ambaye ni mmoja wa waigizaji wa wakuu wa filamu hii na mmiliki wa Twaleb Entertainment
Lucy Komba, Abou na Rashel
 Lucy Komba, Jean Claud na Rashel Scharp
Lucy Komba na Abou wakiwa kama mke na mume katika filamu ya African Boy
Moja ya vitu vinavyovutia katika filamu hii ni waigizaji wa filamu hii kuvaa mavazi ya kiafrika katika baadhi ya scenes licha ya wao kuwa ulaya ambako ni ngumu kupata mavazi hayo lakini watengenezaji wa filamu Tanzania inakuwa nadra sana kwa waigizaji wakuu kuvaa nguo za kiafrika licha ya kuwa zimejaa tele kwasababu uzungu umewekwa mbele mno pasipo kujua hata huko ulaya na marekani mavazi ya kiafrika bado yanavaliwa na baadhi ya watu. Kwenda na wakati sio kuvaa mavazi ya kimagharibi pekee watengenezaji wa filamu Tanzania be creative we have lots to show the world through our movies!

wakijiandaa na script........
wife and husband in black and white.........

get prepared for your original copy....

Follow us on twitter Swahili World Planet  and Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies SWP for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities, features, beauty, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news

No comments:

Post a Comment