Tuesday, October 1, 2013

ACTRESS IRENE UWOYA AACHANA NA UIGIZAJI WA FILAMU.

Actress maarufu Swahiliwood Irene Uwoya amesema kuwa kwasasa anaachana kwanza na uigizaji wa filamu ili kujikita zaidi katika kipindi chake cha Tv ambacho kinahusika na kukarabati nyumba za watu ambazo zipo katika hali duni. Uwoya amesema kuwa uamuzi huo aliuchukua miezi sita iliyopita na tangu hapo hakuingia location kuigiza filamu mpya licha ya kuwa baadhi ya filamu zake mpya bado zinaingia sokoni mpaka sasa. Akizungumza na mtandao wa www.dstv.com Uwoya alisema "Nimeamua kuacha mambo ya movie na kuwaachia wengine, haya maamuzi nimeyafanya kama miezi sita iliyopita… Mara ya mwisho kuigiza ni zaidi ya miezi sita iliyopita pia"

Uwoya alishiriki Miss Tanzania mwaka 2006 na kushika nafasi ya 5 lakini hakuwa maarufu ila baada ya kujiingiza kwenye filamu kwa ushawishi wa Lucy Komba akaanza kuwa star na filamu ya Oprah(2008) aliyocheza na Vicent Kigosi(Ray) na marehemu Steven Kanumba ndiyo ilimfanya ajulikane zaidi nje ya Tanzania. Uwoya ni mmoja wa waigizaji wa Swahiliwood ambao wana mashabiki wengi katika nchi za Afrika mashariki na kati na ameshawahi kuitwa ikulu na baadhi ya viongozi wa nchi hizo.

                                                             Irene Uwoya

Follow us on twitter Swahili World Planet  and Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies SWP for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities, features, beauty, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news

No comments:

Post a Comment