Pages

Sunday, September 15, 2013

ACTOR DR.CHENI ALAMBA DEAL LA KUWA BALOZI WA SIMU MPYA ZA PANTECH.

Dr. Cheni
Muigizaji maarufu wa filamu Swahiliwood Muhsin Awadh(Dr.Cheni) ameteuliwa kuwa balozi wa simu mpya aina ya Pantech ambazo zimeanza kuingia nchini. Muigizaji huyo amesainishwa deal hilo la mwaka mmoja ambapo atakuwa katika matangazo na promotions za simu hizo. Akizungumza na Millardayo Dr. Cheni alisema "Simu inaitwa Pantech, ni simu mpya kabisa na ina operating system ya Android version mpya. Ukizingatia sasa hivi internet ndiyo kila kitu kwenye simu za mkononi, Pantech inatumia 4G na LTE kwenye connection ya internet. Kitu kingine kizuri ni kwamba simu hii ina uwezo wa kujichaji na nguvu za jua. Sasa jua letu hatutalichukia tena na pia ina camera nzuri ambayo inaitwa Spy camera yenye uwezo wa kupiga picha mbali sana"

Star huyo wa filamu za Nipende Monalisa, Jesica na Majanga aliendelea kwa kusema " Majukumu yangu hasa ni kuhakikisha simu hii watu wanatambua uwepo wake. Matangazo na promotion zinapofanyika nitakuwa na shiriki kikamilifu kabisa. Wamenipa mkataba wa mwaka mmoja kwa sasa na swali lako la thamani ya mkataba wangu naomba niweke kapuni kwasasa, ila millardayo.com itakuwa ya kwanza kujua thamani yake muda wa kuweka wazi ukifika. Ninachoweza kukwambia hivi sasa ni bei tu ya simu hizi ambayo ni Tsh 250,000 tu"

Wasanii wengi wakiwemo wa filamu siku hizi wanaanza kufaidi umaarufu wao baada ya kampuni mbalimbali kuanza kufanya nao kazi katika matangazo ya bidhaa zao kama mabalozi, wiki iliyopita Yobnesh Yusuph(Batuli), Rose Ndauka, Slim Omar na Single Mtambalike(Richie) walisainishwa mkataba wa kuwa mabalozi wa wa soko la hisa la Dar es salaam/ Dar es salaam Stock Exchange(DSE), King Majuto na JB ni baadhi ya wasanii wengine wa filamu ambao nao wana mikataba na makampuni katika kutangaza huduma na bidhaa za makampuni hayo.


Katika mkutano na media........................
Follow us on twitter Swahili World Planet  and Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies SWP for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities, features, beauty, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news

1 comment: