Pages

Friday, August 2, 2013

STAMINA AWASHUKIA WASANII WANAOJIHUSISHA NA MADAWA YA KULEVYA.

Stamina ambaye ni  msanii wa hip hop nchini Tanzania na hit maker wa ngoma kibao ambazo zinafanya poa sana, mojawapo ikiwa ngoma yake mpya(Mwambie Mwenzio) aliyofanya na Darasa pamoja na mwanadada Warda anayesoma chuo kikuu cha SAUT Mwanza amesema anakerwa sana na baadhi ya wasanii ambao wamekuwa wakijihusisha na utumiaji au uuzaji wa dawa za kulevya . Msanii huyo amesema inauma sana kuona baadhi ya wasanii wanavyowachambua wenzao kwa kukamatwa na hayo madawa nje ya nchi kitu ambacho kinafanya wasanii wengi waonekane kuwa ni watumiaji wa madawa hayo na kusababisha pia usumbufu kwa wengine pale wanapotaka kusafiri kwenda nje kwa ajili ya show . Stamina ameyasema hayo katika kipindi cha Strengo Saturday kinachorushwa na radio Victoria fm iliyopo Musoma mkoani Mara, wakati akifanya mahojiano na mtangazaji wa kipindi hicho Patrick Derrick Mwankale.

Hiyo ilitokea mara baada ya mazungumzo mengi tu ya utambulisho wa kazi yake hiyo mpya aliyofanya na kina Darasa pamoja na Warda , na mafanikio mengine ya kazi zake kimuziki. Mtangazaji huyo alimuuliza kuhusiana na kashfa zilizopo katika mitandao ya kijamii pamoja na katika vyombo vya habari ,kuhusiana na baadhi ya wasanii kukamatwa na madawa ya kulevya wanapokuwa ughaibuni kupiga show . Stamina alisema " unajua nini Patrick , mimi huwa naumizwa sana na hawa wasanii ambao wanafanya hayo mambo maana wanatufanya hata sisi tusiohusika kuonekana tunafanya hayo pale tunapokuwa nje ya nchi katika shows au katika mambo binafsi. Aliendelea kusema kuwa wasanii wengi wanatamani kuishi maisha ya juu kwa haraka haraka ndio maana unakuta wengi wanapatwa na tamaa ya mambo amabyo hawana uwezo nayo, na mwisho wa siku unakuta wanajiingiza katika biashara ambazo sizo , na mambo yanayowaweka katika hatari kubwa.

 Like our facebook page Swahili World Planet for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities, features, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news.

No comments:

Post a Comment