Pages

Friday, August 2, 2013

WELLU SENGO KUIGIZA PAMOJA NA WEMA SEPETU NA JB BAADA YA TWISTED NA MATILDA.

Latest news ni kuwa actress Wellu Sengo anakuja na filamu kadhaa huku mojawapo akiwa na Wema Sepetu na nyingine akiwa na Jacob Stephen(Jb), ingawa chanzo cha habari hizi hakikuwa tayari kutaja majina ya filamu hizo kwasasa. Ukiachilia mbali filamu hizo ambazo zinatarajiwa kumuimarisha zaidi muigizaji huyo aliyejaaliwa mvuto, Wellu ameigiza pia katika filamu ya Twisted akiwa na Vicent Kigosi(Ray), Hidaya Njaidi na Richard Mshanga(Masinde). Na kwa mara ya kwanza Wellu alionekana katika filamu ya Matilda iliyotoka miezi michache iliyopita mwaka huu akiwa na Hemed na Salma Jabu(Nisha) na alicheza uhusika uliobeba jina la filamu hiyo yaani Matilda.

                                                          Wellu Sengo
 Like our facebook page Swahili World Planet for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities, features, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news.

No comments:

Post a Comment