Pages

Thursday, May 9, 2013

ALI YAKUTI: UVIVU WA KUFANYA TAFITI NDIYO HUWAANGUSHA SCRIPTWRITERS WENGI NCHINI.

Ali Yakuti mmoja wa scriptwriters wachache wanaokubalika Swahiliwood amesema kuwa moja ya vitu vikubwa vinavyopelekea waaandishi wengi wa script nchini kutoa kazi zilizo chini ya kiwango ni kutofanya tafiti na kupata taarifa za kutosha kabla ya kuanza kuandika kazi zao. Yakuti ambaye tayari ameshafanya kazi na watayarishaji wengi wa filamu nchini kama vile Vicent Kigosi(Ray), marehemu Steven Kanumba, Mtitu Game na wengine wengi aliyasema hayo wakati Swahiliworldplanet ilipomuuliza ni sababu gani anafikiri ndizo zinazowaangusha waandishi wengi wa miswada ya filamu kwa kutoa kazi mbovu. Alisema "Ni kwa sababu ya kutokuwa na taarifa za kutosha kwa kile wanachoandika na pia kuwa na uvivu wa kufanya tafiti kabla hawajaandika"

No comments:

Post a Comment