Wiki iliyopita niliwauliza maproducer wawili maarufu wa filamu Swahiliwood kama huwa wanatunza kumbukumbu zote muhimu kuhusu filamu wanazotengeneza lakini walisema sio sana huku wakisema baadhi ya films hawana kumbukumbu kabisa kitu ambacho kilinishangaza sana. Ukweli ni kuwa hizi films zote zilizotengenezwa, zinazotengenezwa na zitakazotengenezwa miaka ijayo zote zitahitajika kuingizwa na kuhifadhiwa katika mtandao maarufu wa Wikipedia na hata vitabu ili kutunza kumbukumbu ambazo zitatumika vizazi na vizazi. Hii si kwa producers tu bali kwa actors wote, directors na wadau wengine muhimu kwenye industry wanahitajika kutunza kumbukumbu zao muhimu ili baadaye wakiingizwa au kuingia kwenye wikipedia basi kuwe na habari zao za kuaminika kutoka kwao wenyewe. katika wikipedia mtu yeyote anaruhusiwa kuongeza au kuondoa habari kama ina ushahidi wa kutosha au kama haina ushahidi wa kutosha lakini mhusika mwenyewe ndiye anatakiwa kuwa primary source.
Ni wazi kuwa filamu nyingi kwa sasa zinatengenezwa Swahiliwood lakini miaka mingi ijayo tasnia ikiwa imekuwa sana zitakuja kurudiwa na vizazi vijavyo kutokana na mahitaji ya muda huo huku story zikiwa kutoka filamu za sasa za Swahiliwood. Hili ni jambo la kawaida sana ambalo tunalishuhudia hata kutoka Hollywood na Bollywood ambao huwa wanatengeneza upya films zilizotengenezwa zamani ili kuziakisi katika vizazi vya wakati husika/sasa lakini original story ikibaki kuwa filamu ya zamani na hii huwekwa wazi kabisa kwa sababu inakubalika professionally. Pia vizazi vijavyo vitahitaji kuwa na kumbukumbu zote muhimu kuhusu waasisi na na waigizaji wote wa films, directors na wengineo. Hivyo basi ni muhimu muigizaji,directors, producers watunze kumbu kumbu za matukio yote muhimu za films zote wanazoigiza au kuzitoa.
Leo hii ukiingia kutafuta film,migizaji, director yoyote kutoka Hollywood au Bollywood utampata wikipedia kwa kuwa huwa wanatunza kumbukumbu muhimu tangu story ya film inaandaliwa ,mpaka film husika inaingia sokoni na na kadiri inavyokuwa sokoni na kuleta matukio mapya huwa yanaandikwa. Mfano ukiingia Wikipedia ukisoma kuhusu Steven Kanumba ni wazi kuwa kuna matukio mengi muhimu hayapo na yanatakiwa kuwekwa ila sijui kama kumbu kumbu zipo, hata matukio muhimu kuhusu maadhimisho ya kifo chake mwaka mmoja tangu afariki dunia yalitakiwa kuwepo siku iliyofuata lakini wapi mpaka sasa hakuna updates zozote kitu ambacho sio kizuri hata kidogo maana vizazi vijavyo vitashindwa kujua mchango wake kwa undani katika films za kiswahili. Tuanze kuchukua hatua sasa.
The late Steven Kanumba
No comments:
Post a Comment