Pages

Monday, April 22, 2013

JACKLINE WOLPER: MIMI NA RAMMY GALIS SIYO WAPENZI BALI TUNAFANYA FILAMU YA KIISLAMU PAMOJA.

Tangu juzi baadhi ya blogs zimeandika kuwa Jackline Wolper na muigizaji mwenzake Rammy Galis wanaonekana kuwa wapenzi wapya kwa picha za wawili hao kuonekana katika mitandao ya kijamii huku zikiambata na maneno ya my baby. Juzi Swahiliworldplanet ilipoona tu picha za wawili hao ilimuuliza Wolper na kudai kuwa wao si wapenzi bali wanafanya filamu ya kiislamu, tukamuuliza tena filamu inaitwaje but Wolper hakujibu kwa wakati akionekana kuwa busy kidogo na mambo flani. Ila baada ya kuona news zinasambaa sana kuwa wawili hao wanakula bata kisirisiri SWP ilimuuliza tena Wolper kuhusu madai hayo na kusema si kweli ila wanafanya filamu kama alivyosema mwanzo na filamu hiyo akasema inaitwa Kanzu na Hijabu Zaficha Maovu. Wolper alisema "bata gani si tunafanya filamu ya kiislamu, inaitwa Kanzu na Hijabu Zaficha Maovu". Hayo ndiyo majibu ya Wolper kama kweli ni wapenzi kama wengine wanavyodai itakuja kubainika tu maana wahenga wanasema penzi ni kikohozi hivyo huwezi kukizuia. Rammy Galis anaonekana katika films kama Malaika akiwa na Seth Bosco na Rose Ndauka. Hatukufanikiwa kumpata haraka Rammy ili kutoa maoni yake kuhusu issue hiyo lakini tukimpta utasikia from his side too.

                                                                        Rammy Galis
                                                              Jackline Wolper

No comments:

Post a Comment