Monday, April 8, 2013

IRENE UWOYA NA DIAMOND WAKWAA SKENDO MPYA YA KULALA PAMOJA HOTELINI.

Mtandao wa Globalpublishers umeripoti kuwa Tanzanian top singer Diamond Platinumz and Swahiliwood famous actress Irene Uwoya walilala pamoja baada ya kunaswa na kamera za magazeti hayo maarufu kwa kufuatilia skendo za mastaa wa bongo. Uwoya na Diamond walinaswa tarehe 25 mwezi uliopita katika hoteli moja ya hadhi ya nyota tano maeneo ya mbezi beach wakiingia usiku wa saa mbili hivi na kutoka kesho yake mchana kumaanisha walilala pamoja huku picha zikiwaonyesha hatua kwa hatua. Hii ni skendo mpya kwa mastaa hao ambapo Uwoya ni mke wa Mtu na hivi karibuni alisema wamerudiana na Ndikumana baada ya kutengana kwa muda Uwoya akidaiwa kuwa ndiye chanzo kwa kutotulia kwenye ndoa yake.

Kwa upande mwingine Diamond nae ambaye anaidaiwa kutembea na mastaa wa kike kibao ni hivi karibuni tu alidaiwa kuwa katika uhusiano mpya na Penny ambaye ni mtangazaji na inasemekana Penny ni mjamzito na Diamond mwenyewe alikiri kuwa ni kweli na kampa gari la kuendea clinic. Hata hivyo Globalpublishers wamechelewa kidogo kuitoa habari hii ambayo wameitoa leo April 8 katika gazeti la Ijumaa Wikienda ikionekana kuwa walikuwa katika uchunguzi mzito wa habari hiyo ili kupata vielelezo vya kutosha kabla ya kuitoa na tayari wameitoa kuonyesha wana kila sababu ya ushahidi. Uwoya ni makamu mwenyekiti wa klabu ya Bongomovie Unit hivyo skendo hiyo inamuweka rehani katika klabu hiyo iliyoapa kuwashughulikia members watakaoichafua kwa skendo. Kusoma habari ya Globalpublishers kuhusu wawili hao ingia hapa......
www.globalpublishers.info . Angalia picha gazetini zikiwaonyesha wawili hao hatua kwa hatua.




                                                           Uwoya na Diamond


No comments:

Post a Comment