Pages

Tuesday, April 23, 2013

DIAMOND AKIRI KUMREKODI WEMA, AKATAA KUSAMBAZA CLIP, APOTEZEA KUMUOMBA MSAMAHA LIVE.

Baada ya kudaiwa kumrekodi Wema Sepetu akimuomba warudiane na kusambaza clip katika radio Diamond amefunguka na kusema ni kweli alimrekodi Wema kwa kuwa alikuwa akitaka kumgombanisha na mpenzi wake wa sasa Penny na Penny alikuwa hamuamini Diamond hivyo kuamua kumrekodi Wema ili Penny ajue kila kitu lakini amekana kuhusika kuisambaza clip kitu ambacho wengi hawakiamini bado wanaamini ni yeye kwa kuwa huko nyuma tayari ana historia ya kumdhalilisha mnyange huyo, na alipotakiwa kumuomba msamaha live Wema mwanamuziki huyo alikataa na kusema hana kosa. "“Lengo langu kubwa ilikuwa ni kurekodi sauti hiyo  na kumsikilizisha Penny, sasa ambaye aliichukua na kuisambaza mitaani sijui ni nani, lakini hata mi sikujisikia vizuri nilipoisikia mitaani maana sikupenda hali iwe hivyo lakini ndo sina jinsi”.

Issue ya mwanamuziki huyo kumrekodi Wema na clip kusambaa katika media ilifanya watu wengi wamponde sana mwanamuziki huyo na mpenzi wake wa sasa Penny huku wanawake wengi wakichukizwa na kitendo alichofanyiwa Wema kuwa hakikua kizuri wala kisingeweza kufanywa na mtu mzima aliyeelimika na anayejali mambo yake private, Diamond na Penny walifananishwa na malimbukeni na watu wasiojielewa bali kutaka umaarufu usio na tija kwani mambo hayo wangeyamaliza kisiri bila kufika kwenye media.


No comments:

Post a Comment